Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mama Anne Makinda amesema umefika wakati kwa Watanzania kuwekakipumbele katika suala la afya kwa kujiunga na mfumo wa bimaya afya unaowahakikishia upatikanaji wa huduma za matibabuwakati wote.
Mama Makinda ameyasema hayo leo (Alhamisi 2Mei,2020) wakati akizindua mpango wa Machinga Afya ambaounawalenga wamachinga wote nchini kwa gharama nafuu yashilingi 100,000 kwa mwaka.
“Afya ni muhimu kuliko jambo lolote, ni wakati wa kuwekakipaumbele kwa kuhakikisha tunakuwa na bima ya afya badalaya kuelekeza nguvu nyingi katika kuchangia harusi na sherehezingine ambazo zinahitaji kwanza afya yako iwe njema,” alisema Mama Makinda.
Alisema kuwa tendo la uzinduzi huo ni matokeo chanya ya kazikubwa iliyofanywa na Mfuko kuhakisha kila kundi la wananchilinakuwa na fursa ya kujiunga na huduma za matibabu.
Alisema kuwa kauli ya HAPA KAZI TU iliyotolewa mwaka 2015 na Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli imekuwa na matokeomakubwa sana ambayo kila mmoja kwa sasa anaweza kuyaonakwa macho.
“Wakati hii kauli ikitolewa ilikuwa ni ngumu kuielewa lakinikwa sasa unaweza kuielewa kwa kuunganisha matukioyanayoendelea mfano tumeona mambo makubwa ambayo Raiswetu Dkt. Magufuli ameyafanya katika sekta zote na tumeonahata ambavyo amesimama na Watanzania kwenye hiki kipindikigumu cha CORONA hali ambayo imeondoa hofu na watuwameendelea kufanya kazi zao kama kawaida,” alisema.
Alisema kuwa Serikali imefanya kazi kubwa ya uboreshaji wahospitali nchini na huduma za matibabu kwa ujumla hatuainayowezesha upatikanaji wa huduma zote za matibabu kirahisina kuondoa changamoto zilizokuwepo awali zikiwemo zaukosefu wa dawa.
“Mfuko umejipanga sana kuwahudumia wananchi na kuwafikiakatika maeneo yao, hivyo natoa wito kwa watoa hudumakuhakikisha wanawahudumia wanachama kulingana na maadiliyao ya kazi,” alisema Mama Makinda.
Naye Mwenyekiti wa Wamachinga Tanzania Bw. Stephen Lusinde akizungumza katika hafla hiyo, amesema kwambakitendo cha kuzinduliwa kwa mpango huo ni sawa na Machingakuzaliwa upya wakiwa na matumaini ya ulinzi wa afya zao.
“Hakika siku ya leo kwetu ni sawa na kuzaliwa upya, hapo awalihatukuwa na uhakika wowote wa ulinzi wa afya zetu, kupewafursa hii na Mfuko inatuhakikishia usalama zaidi wa mitaji yetulakini uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote,” alisem Bw. Lusinde.
Alitumia fursa hiyo kutoa pongezi zake kwa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa namnaambavyo amehakikisha chini ya uongozi wake kunakuwa nauhakika wa huduma zote za kijamii ikiwemo suala la afyaambalo ni suala nyeti.
“Miaka ya nyuma sisi tulijiona kama ni kundi ambalolimetengwa lakini kwa kitendo hiki cha sisi kuanza kutumiahuduma za NHIF sasa tunatembea kifua mbele na katika hilinaomba niwapongeze sana Mfuko kwa kuhakikisha hililinafanikiwa na Wamachinga wote nchini wamepokea hili kwafuraha kubwa,” alisema Bw. Lusinde.
Akielezea namna Mfuko ulivyojipanga kutoa huduma kwakundi hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Kongaamesema mkakati uliopo ni kutoa huduma bora kwa wanachamana kuendelea kuwafikia wananchi ili waweze kujiunga.
“Leo tunaanza na kundi la Wamachinga wa Kariakoo ambaowana utaratibu mzuri sana wa kuratibu wanachama wao nampango huu umelenga kuwawezesha wajasiliamali hawa kwagharama ya shilingi 100,000 tu kwa mwaka hivyoniwahakikishie kuwa upatikanaji wa huduma ni wa uhakikakabisa,” alisema Bw. Konga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...