Tume ya uchaguzi nchini Burundi imemtangaza mgombea wa chama tawala Meja Jenerali Evariste Ndayishimiye kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika juma lililopita.
Meja Jenerali Ndayishimiye ameshinda kwa kupata 68.72% ya kura zilizopigwa, wakati Agathon Rwasa, kutoka chama kikuu cha upinzani akipata 24.19% , kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na tume hiyo.
Kwa kuwa Meja Jenerali Ndayishimiye amepata zaidi ya 50% ya kura, ameepuka kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi.
Haya ni matokeo ya awali ya uchaguzi , ambapo matokeo ya mwisho yatatangazwa na mahakama ya kikatiba tarehe 4 mwezi Juni.
Meja Jenerali Ndayishimiye aliteuliwa kupeperusha bendera ya chama cha CNDD-FDD katika kikao kisicho cha kawaida kilichofanyika Gitega, mji mkuu wa kisiasa baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa saa tatu ya chama tawala cha CNDD-FDD.
Wagombea wengine waliochuana
kwenye kinyang'anyiro hicho ni pamoja na;
Gaston Sindimwo (Uprona) - 1.64%
Domitien Ndayizeye (Kira Burundi) - 0.57%
Léonce Ngendakumana (FRODEBU) - 0.47%
Nahimana Dieudonné - 0.42%
Francis Rohero - 0.20%
HABARI KWA HISANI YA BBCSwahili.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...