NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA
Mbunge wa Jimbo la
Mkuranga na Naibu wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega
amekabidhi Magodoro Sabini (70) kwa ajili ya kambi ya watu walioko
kwenye karantini wilayani Mkuranga.
Hatua hiyo ya Ulega
ni kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali za kupambana na ugojwa
wa Homa ya Mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona ambao umekuwa
janga la Ulimwengu.
Magodoro hayo, Mbunge
huyo aliyapokea kutoka kwa wadau na marafiki mbalimbali walioamua
kuunga mkono jitihada za serikali kupambana dhidi ya corona.
Akipokea magodoro
hayo ,mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga alimshukuru Mbunge Ulega
kwa jitihada hizo na amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono
juhudi hizi za serikali za kupambana dhidi ya corona.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...