WAZIRI wa Maji, Prof. Makame Mbarawa (Mb) amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA).
Taarifa ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo imemtaja aliyeteuliwa kuwa ni Mhandisi Tamimu Twaha Katakweba. Aidha, kufuatia uteuzi huu Mhandisi Katakweba anakuwa Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi wa MORUWASA.
Uteuzi huu umefanyika chini ya Sheria Namba 5 ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019.
Kitengo cha Mawasiliano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...