Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo May 06 ametoa Saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es salaam "kula bata" kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo watakamatwa kwa kosa la Uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura Usiku.

RC Makonda amesema  Mbunge anaepaswa kuwa Dar es salaam ni yule mwenye Kibali au Ruhusa ya Spika wa Bunge tofauti na hapo ni vyema wakafunga virago vyao na kurudi Bungeni ili kuepuka kukamatwa.

"Hakuna asiefahamu kuwa sasahivi tuko katika Mapambano dhidi ya Virusi vya Corona na sio uzururaji, ifahamike huu sio Mji wa wazururaji hivyo natoa Masaa 24 kwa Wabunge wote kurudi Dodoma tofauti na hapo tutawakamata kwa kosa la Uzururaji kama tunavyowakamata Machangudoa" alisema RC Makonda

Aidha RC Makonda amesema kwa Sasa ni kipindi muhimu cha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali na wananchi waliwachagua kwenda kuwawakilisha Bungeni na kupigania maslahi yao hivyo kitendo cha kukimbia Vikao vya Bunge ni kutowatendea haki wananchi waliowachagua.

Hata hivyo RC Makonda amesema kinachomshangaza ni kuona Wabunge hao wamekimbilia Dar es salaam kufurahia Maisha badala ya kwenda Majimboni mwao kutembelea wananchi wanaokabiliwa na Mafuriko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...