Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipokea hundi ya Sh. 50,000,000/= kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha nguzo ya Qwihaya General Enterpises Co. Limited, Leonard Mahenda, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mai 4, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipokea hundi ya Sh. 50,000,000/= kutoka kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya kuzalisha nguzo ya Mufindi Woodpoles Plant and Timber Limited, Salim Ahmed Abeid, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 4, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipokea hundi ya Sh. 50,000,000/= kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya kuzalisha nguzo ya POLES (T) Limited, Salim Bisher Huwel, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 4, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza kwenye makabidhiano ya hundi tatu zenye thamani ya Sh. 150,000,000/= , zikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwawa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 4, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza kwenye makabidhiano ya hundi tatu zenye thamani ya Sh. 150,000,000/= , zikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwawa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 4, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza baada ya kupokea hundi tatu zenye thamani ya Sh. 150,000,000/=, zikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 4, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amepokea msaada wa hundi tatu zenye thamani
ya sh. milioni 150 zilizotolewa na kampuni tatu zinazozalisha nguzo za umeme
nchini kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa
na virusi vya Corona (COVID- 19).
Waziri
amepokea michango hiyo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe
4 Mei, 2020 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa, Jijini Dodoma. Michango hiyo
imetolewa na kampuni Mufindi Woodpoles Plant and Timber Ltd, Qwihaya General
Enterprises Co Ltd na Poles (T) Ltd ambapo kila kampuni imetoa sh. milioni 50.
Akizungumza
wakati wa kupokea michango hiyo Waziri Mhagama aliwapongeza viongozi wa kampuni
hizo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha inapambana na
janga la ugonjwa wa COVID-19.
“Nawashukuru
sana kwa niaba ya Serikali na hii inaonesha uzalendo, utayari na kuhakikisha
kila Mtanzania anakuwa ni sehemu ya mapambano hayo kwa vitendo,”alieleza Waziri
Mhagama.
Pia,
Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo kuwasihi wakandarasi wengine pamoja na
Watanzania kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kujitolea kwa hali na mali
ili kuwezesha katika kukabiliana na janga hilo.
“Tunatoa
wito kwa Watanzania wote kuona umuhimu na kuguswa na janga hili kwa kuchangia
kwa kadiri inavyofaa ili kuendeleza uzalendo kwa hali ya kujali na kuonesha
utayari ili kudumisha hali ya utamaduni uliopo tangu awali wa umoja na
mshikamano ,”alisema Waziri Mhagama.
Aliwahakikishia
wadau hao kuwa, michango hiyo itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kuwaeleza
kuwa imefika katika eneo salama.
Awali,
Waziri wa Nishati Dkt. Medadi Kalemani aliwapongeza viongozi wa kampuni hizo
kwa michanga waliyoitoa kwa Serikali ambayo inakwenda kuongeza nguvu katika
kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.
“Niwapongeze
wakandarasi hawa kwa kuonesha nia ya kushiriki katika mapambano haya na wito
wangu kila anayeguswa na janga hili ni faraja kubwa mnayoitoa kwa Serikalini
katika kuhudumia na kusaidia katika kipindi hiki. Pia nawaomba wakandarasi
wengine waige, ”alisema Dkt. Kalemani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...