Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
LINAPOKUJA
suala la kutengeneza fedha sio kila mtu atatengeneza fedha kwa njia
halali, baadhi ya wahalifu ulimwenguni wamefahamika zaidi kutokana na
umiliki wao wa pesa nyingi zilizopatikana kwa njia isiyo ya halali,
wengi wao wamekuwa wakipata pesa kupitia biashara haramu ikiwemo uuzaji
wa dawa za kulevya, kuendesha mitandao ya ngono, uuzaji wa binadamu,
ujangili na hata kutumia silaha ili kujipatia mali.
Licha
ya shughuli zao kuwaweka katika hatari kubwa baadhi ya wahalifu
wameweza kutengeneza kiasi kikubwa cha fedha ingawa hawawezi kufurahia
fedha hizo kwa uhuru ukilinganisha na wananchi wa kawaida.
Baadhi ya wahalifu waliotengeneza kiasi kikubwa cha fedha ni pamoja na;
Carlos Enrique Lehder Rivas (dola bilioni 2.7)
Ni
mwanzilishi mwenza genge la dawa la kulevya la Medellian Cartel na
alianza kazi ya uhalifu kwa kuuza magari ya wizi, bangi na mwishowe
Cocaine pia alisimamia vikosi vya genge vya wamiliki bunduki, boti,
helikopta, mashamba ya mbio za farasi na kundi lake la Neo-Facist.
Alikamtwa
na kuhukumiwa kifungo cha maisha bila msamaha na miaka 135 ambayo
ilipunguzwa hadi kufikia 55 na bado yupo chini ya uangalizi huko
Marekani.
Khun Sa (dola bilioni 5)
Kuanzia
mwaka 1974 hadi 1994 Khun alijulikana sana kama mpenda dawa wa kulevya
na mwongozaji magenge ya uharifu, alifanya biashara ya silaha ili
kujipatia ulinzi.
Mwaka1996
alijisalimisha katika Mamlaka za ulinzi huko Burma kwa sharti la kupewa
ulinzi toka kwa Serikali na mwaka 2007 akiwa na miaka 73 alifariki
dunia kwa sababu zisizoeleweka.
Viktor Bout (dola bilioni 6)
Bout
alishtakiwa kwa tuhuma za mauaji dhidi ya maafisa wa Marekani,.
Kushirikiana na kundi la ugaidi la FARC, udanganyifu pamoja na
utakatishaji fedha ili akuze biashara yake, mwaka 2012 alihukumiwa
kifungo cha miaka 25.
Amado Carillo Fuentes ( Dola milioni 25)
Huyu
anatajwa kuwa tajiri wa pili katika genge la wauza dawa za kulevya,
amekuwa akisambaza dawa hizo katika mataifa ya Marekani, Mexico na
Columbia, alifariki mwaka 1997 baada ya upasuaji wa kubadili mwonekano
wake kushindikana na baadaye daktari aliyefanya upasuaji huo alikutwa
amekufa huku akiwa amefungwa katika chuma na ilielezwa kuwa aliteswa
kabla ya kuuwawa.
Pablo Emilio Escobar (Dola bilioni 30)
Anafahamika
zaidi kwa jina la "Father of Cocaine" akiwa na miaka 35 alikuwa mmoja
wa watu watajiri zaidi duniani, licha ya kutofahamika kwa kiasi
alichokitengeneza inakaridiwa alikuwa na umiliki wa dola za kimarekani
bilioni 30, imeelezwa kuwa Pablo amekuwa akisambaza asilimia 80 ya dawa
za kulevya nchini Marekani katika miaka ya 80 huku ikikadiriwa alikuwa
akitengeneza dola za kimarekani 420 kwa wiki, alifariki mwaka 1993.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...