Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
KATIKA kuadhimisha Siku ya Vipimo Duniani, Mkurugenzi wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Stella Kahwa amesema kuwa Wakala huo upo sehemu zote hapa nchini kuhakikisha Vipimo katika Malighafi na bidhaa mbalimbali vinatumika na kuzingatiwa kwa usahihi.

Stella ameyasema hayo leo, May 20, 2020 jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho hayo yenye Kaulimbiu ya Vipimo katika Biashara ya Kimataifa. “Tanzania ni nchi ambayo inafanya Biashara kubwa nchi mbalimbali, vipimo vinatumika katika Malighafi na Bidhaa zilizotengezwa, kwa hivyo lazima tuzingatie vipimo sahihi”, amesema Bi. Stella.

Stella amesema WMA katika Sekta ya Usafirishaji wanahakikisha wanakagua Mizani ya TANROAD ili kuiweka miundombinu katika ubora na kuwapa fursa wakulima katika usafirishaji bidhaa na mazao yao kwa uhakika, amesema WMA inasimamia pia Sekta ya Mafuta katika Biashara za Kimataifa kuhakikisha vipimo vipo sahihi.

Amesisitiza kuelekea Uchumi wa Viwanda, WMA inahakikisha bidhaa zinapimwa kwa usahihi kutoka inapokuwa Malighafi hadi inapofika Kiwandani kwa ajili ya kutengeneza Bidhaa, amesema Miradi ya Ujenzi ambayo Serikali inasimamia kwa sasa kila bidhaa inayotumika inapimwa kwa usahihi.

“Katika Sekta ya Afya, WMA tunahakikisha mizani inayotumika Mwananchi, anapimwa kwa usahihi na kupata vipimo sahihi ili apate Dawa kwa kipimo kinachotakiwa”, amesema Stella.

Kwa upande wake, Meneja wa Mawasiliano, Wakala wa Vipimo (WMA),  Irene John ameishukuru Serikali kuwapatia Vifaa vya kisasa katika kuhakikisha biashara za kimataifa za Madini kwa Wachimbaji wa Wakubwa, Wa kati na wadogo wanapata haki yao ya vipimo sahihi na kuiletea Serikali pato la Kodi.
Mkurugenzi wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Stella akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yanayofanyika kila mwaka May 20, katika maadhimisho ya mwaka huu Kaulimbiu ni Vipimo katika Biashara ya Kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...