Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ludewa (Kulia) akishirikiana na wananchi kuchimba barabara inayotoka kata ya Mbwila kwenda Lifuma.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ludewa(Kulia) akiwa na baadhi ya wananchi wakipita katika barabara baada ya kumaliza zoezi la uchimbaji.
Wananchi wakikata ikiwa ni harakati ya kut engeneza barabara
Wananchi wa kata ya Mbwila na Lifuma wakichimba barabara

Na Shukrani Kawogo
Mwenyekiti wa halmashauri ya Ludewa Edward Haule akiambatana na madiwani wa kata mbalimbali,wenyeviti wa vijiji wa kutoka kata ya Mbwila na Lifuma pamoja na wananchi wa kata hizo wameungana kwa pamoja katika uchimbaji wa barabara ya kuunganisha kata hizo.
Akizungumzia zoezi la uchimbaji wa Barabara hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri Bw. Haule alisema kuwa wazo hilo lilitolewa na wananachi wenyewe na kukaa na viongozi ambapo walifanya makubaliano ya kujumuika kuchimba barabara hiyo kwa nguvu zao ambayo inaurefu wa zaidi ya kilometa 20 na wanatarajia kuchimba kwa muda wa miezi sita hadi 12.
Alisema barabara hiyo itakapokamilika itakuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa kata hizo mbili na hata kwa watu wengine kwakuwa wamekuwa wakipata wakati mgumu sana katika kufikisha huduma kwa kata ya Lifuma.
“Hii barabara itakuwa ni msaada mkubwa sana hasa kwa wakazi wa Lifuma kwakuwa wamekuwa wakishundwa kufikiwa na huduma za msingi kama huduma za afya hasa inapotokea dharula”. Alisema Mwenyekiti.
Naye diwani wa kata ya Lifuma Herbet Haule amesema kuwa wameungwa mkono na wadau mbalimbali wa maendeleo ambapo wamechangia kiasi cha fedha za kitanzania ml. 1, 225,000moja ambazo zimesaidia katika matumizi mbalimbali ya uchimbaji huo.
Aliongeza kuwa katika fedha hizo laki nane na elfu thelathini na tano zimetumika kununu vifaa mbalimbali vya uchimbaji na laki tatu na tisini kwa ajili ya chakula.
Aidha kwa upande wa wananchi wamefurahishwa kwa hatua hiyo ya uchimbwaji wa barabara na kusema kuwa itawasaidia kurahisisha shughuli zao na kuwawezesha kupata huduma ya afya kwa urahisi na wameiomba serikali kuwaunga mkono katika zoezi hilo ili kuifanya barabara hiyo kuwa bora zaidi.
“Hii barabara ni msaada mkubwa sana kwetu kwani tumekuwa tukipata shida katika kuwafikisha wagonjwa mjini kupata matibabu pia usafirishaji wa bidhaa za kutoka ziwani kuja mjini kama samaki n.k na kutoka mjini kuja ziwani kama vinywaji n.k”. Walisema wananchi.
Zoezi hilo la uchimbaji barabara litakuwa linafanyika kwa wiki mara moja ambapo kila siku ya juma nne wananchi watalazimika kusimamisha shughuli zao na kwenda kuungana kwa pamoja katika kuendeleza uchimbaji huo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...