Na Fedson Masawa-Jimbo la Musoma Vijijini
Msaidizi wa Mbunge
WANAKIJIJI
cha Kijiji cha Kiemba, Kata ya Ifulifu wameendelea kushirikiana na
WADAU wa MAENDELEO kuboresha MIUNDOMBINU ya SHULE YA MSINGI MURUNYIGO
iliyofunguliwa Mwaka 1956.
Hivi karibuni BENKI ya CRDB imechangia ukamilishaji wa ujenzi wa chumba kimoja cha DARASA kwenye Shule hiyo.
MWALIMU
MKUU wa Shule hiyo, Mwl Grace Majinge amesema kwamba jumla ya WANAFUNZI
Shuleni hapo ni 846, na mahitaji ya VYUMBA vya MADARASA ni 21,
vilivyopo ni 9 na UPUNGUFU ni 12.
BENKI ya CRDB imechangia kupunguza UPUNGUFU huo kwa kutoa VIFAA vya UJENZI vya kukamilisha CHUMBA kimoja (1) cha DARASA.
AFISA
MTENDAJI wa Kijiji hicho, Ndugu Regina Mafuru Chirabo ameorodhesha
VIFAA vilivyochangwa na CRDB kuwa ni: SARUJI MIFUKO 60, RANGI NDOO 2 na
KOPO 1, SQUARE PIPE 5, FLAT BAR 10, SHEET 1, KOMEO na BAWABA.
AFISA
MTENDAJI huyo na WANANCHI wa Kijiji cha Kiemba na VIONGOZI wengine,
wakiwemo DC, DED na MBUNGE wa Jimbo WAMEISHUKURU sana BENKI ya CRDB kwa
MCHANGO huo na kwa pamoja wameahidi kukamilisha ujenzi huo kabla ya
tarehe 30 Mei 2020.
MWENYEKITI
wa Serikali ya Kijiji cha Kiemba, Ndugu Rocket Mauna Rukiko ameungana
na WANAKIJIJI wenzake KUSHUKURU WADAU wengine wa MAENDELEO
waliokwishachangia UJENZI kwenye Shule hiyo, ambao ni: SERIKALI, PCI na
MBUNGE wa JIMBO lao.
SERIKALI
inaendelea kugharamia UBORESHAJI wa Elimu kwenye Shule hiyo. MRADI wa
EQUIP wa SERIKALI yetu nao umechangia sana UBORESHAJI wa Elimu Shuleni
hapo.
PROJECT CONCERN
INTERNATIONAL (PCI) imejenga VYOO vya S/M Murunyigo. Imetoa CHAKULA cha
WANAFUNZI, VITABU, ELIMU ya AFYA na inaendelea kuchangia UBORESHAJI wa
ELIMU kwenye Shule hiyo.
MBUNGE
wa JIMBO la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amechangia Shule
hiyo ifuatavyo: SARUJI MIFUKO 60, MADAWATI 106 na VITABU vingi vya
MAKTABA.
OMBI KUTOKA KWA WANAVIJIJI
KIJIJI
cha Kiemba, Kata ya Ifulifu kinawaomba WADAU wa MAENDELEO wakiwemo
WAZALIWA wa Kijiji na Kata hiyo KUCHANGIA ujenzi wa Miundombinu ya Shule
yao ya Msingi iliyoanzishwa Mwaka 1956.
Picha
zilizoko hapa zinaonesha baadhi ya WANANCHI wa KIJIJI cha KIEMBA, Kata
ya Ifulifu wakiwa kwenye kazi za ujenzi wa MIUNDOMBINU ya S/M MURUNYIGO.
Ofisi ya Mbunge
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...