Na Al-Hassan, Michuzi TV

WASAFI Redio wameamua!Ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya watangazaji wa kipindi cha the switch kinachorushwa na Wasafi Redio pamoja na Wasafi TV kuamua kuitoa gari aina ya Altezza kwa ajili ya kushindaniwa na wasikilizaji wao ikiwa ni sehemu ya kutimiza ndoto za vijana walio wengi ambao wanaamani kumiliki gari hiyo.

Hivyo ili kushinda gari hiyo , wasikilizaji wa Wasafi Redio, Wasafi TV pamoja na wale wanaofuatilia mitandao ya kijamii ya Wasafi watatakiwa kusikiliza vipindi mbalimbali ambavyo vitakuwa vikirushwa hewani muda wote na kupitia vipindi hivyo kutakuwa na maswali yanayoulizwa na watangazaji wa vipindi.

Akizungumza leo wakati wa kuitangaza gari hiyo inayoshindaniwa na wasikizaji wao, Mtasharishaji na Mtangazaji wa kipindi cha the switch Lily Ommy amesema kuwa wasikizaliaji wao watatakiwa kufuatilia tu vipindi mbalimbali vya redio na TV na kisha kutakuwa na maswali.

"Tumekuja kubadilisha maisha ya kijana wa kitanzania, tumekuja kufanikisha ndoto za vijana wa Tanzania kwani tunafahamu vijana wengi wanapenda kumiliki magari ya ndoto zao na walio wengi wanapenda kumiliki Alteza. Kila kijana mtaani anaizungumzia Alteza kama gari ya ndoto yake, kwa hiyo the switch imekuja kubadilisha maisha ya vijana kabisa,"amesema Lil Ommy.



Amesisitiza ili kushinda gari hiyo msikilizaji anatakiwa kusikiliza 88.9 Wasafi ."Huwezi kujua swali litatoka kipindi gani, hivyo ni kusikiliza redio na mitandao ya kijamii wakati wote.Gari ni ya vijana wote na mshindi wa gari atakapopatikana basi namba ya usajili wa gari litaandikwa jina lake .Ndio maana kwa sasa haina namba wala jina , inasubiri mwenyewe.

Akifafanua zaidi Lil Ommy amesema kuwa kampeni ya kushindanisha gari hiyo itakuwa kwa muda wa mwezi mmoja na walengwa ni vijana wenye kuanzia umari wa miaka 18-30 na kwamba kampeni hiyo imepewa jina la Teleza na Tezza.

"Kama nilivyosema awali mshindi ni yule ambaye atafanikiwa kujibu maswali yatakayokua yanaulizwa kwenye kipindi na kuwapa fursa wasikilizaji kupiga simu na kujibu maswal."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...