Na Vero Ignatus, Arusha

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha linawashikilia Waandishi  wawili raia wa  nchi jirani ya Kenya kwa kosa la kuingia nchini bila kibali

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Clinton Isimbu( 22)kabila Mluya,mpiga picha wa Elimu Tv ya Kenya,mwingine ni Kaleria Shadrack(23)kabila mmeru ambaye pia ni mwandishi wa habari Elimu Tv ya nchini Kenya.

Kamanda Shana amesema watuhumiwa hao waliingia nchini kwa njia ya Panya,ambapo kwa Sasa wote wawili wamekabidhiwa kwa  Idara ya Uhamiaji mkoa wa Arusha kwa hatua zaidi za kisheria.

Aidha watuhumiwa hao walikamatwa tarehe 16/5/2020 majira ya 13:30hrs maeneo ya mtaa wa kisongo kata ya Namanga,tarafa ya Longido.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...