
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akioneshwa na
kupewa maelezo kuhusu mtambo wa kuzalisha mvinyo kutoka kwa Mhandisi wa
Kemikali na Mchakato tija wa kiwanda hicho, Daniel Mollel wakati wa
ziara yake katika kiwanda cha kuzalisha mvinyo cha DOMIYA.

Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akipokea maelezo
ya vifaa vilivyomo katika vyumba vya kulala wageni katika hoteli ya
DOMIYA kutoka kwa Meneja Mkuu wa hoteli hiyo alipofanya ziara yake ya
kikazi.

Meneja Mkuu wa
eneo la uzalishaji la DOMIYO ESTATE Bi. Katrini Mwimbe akimuonesha
mazingira ya eneo hilo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji)
Mhe. Angellah Kairuki alipotembelea kukagua uzalishaji wa vinywaji
vikali na baridi vinavyozalishwa kiwandani hapo.

Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiangalia maji
yanayozalishwa na kiwanda cha ASANTE wakati wa ziara yake kiwandani hapo
wa kwanza kulia ni Meneja Mkuu wa kiwanda hicho Bi. Katrini Mwimbe.

Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akipokea maelezo
kuhusu kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji bariki ikiwemo maji, juisi na
soda aina ya ASANTE kutoka kwa Meneja Mkuu wa kiwanda hicho Bi. Katrini
Mwimbe alipofanya ziara kiwandani hapo tarehe 23 Mei, 2020.Kiwanda hicho
kipo eneo la Chinyoya Dodoma.

Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki atoa majumuisho
ya ziara yake katika eneo la uzalishaji la DOMIYO ESTATE lililotengwa
kwa ajili ya kuzalisha mvinyo, vyumba vya kulaza wageni, kiwanda cha
vinywaji baridi mara baada ya ziara ya kukagua shughuli zinaoendelea
katika eneo hilo wakati wa ziara yake kijiji cha Chinyoya Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
*******************************
MWANDISHI WETU
Waziri wa nchi
Ofisi ya Waziri ya Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angellah
Kairuki amewatoa hofu wawekezaji na wafanyabiashara juu ya changamoto
mbalimbali zinazowakabili.
Azingumza
mwishoni mwa wiki Jijini Dodoma, wakati wa ziara yake ya kukagua
shughuli za uzalishaji katika viwanda vinavyozalisha mvivyo kikiwemo
DOMIYA ESTATE kinachozalisha vinywaji vikali na baridi kama soda, maji
na chai baridi aina ya ASANTE na kiwanda cha Alko Vintages Co. Ltd
amesema kuwa Serikali ina mipango na mikakati ya kuhakikisha kuwa kuna
mazingira bora ya uwekezaji.
“Serikali
inatambua changamoto mnazopitia na imeweka mikakati ya kuhakikisha
inazitatua ikiwemo uanzishwaji wa sheria mpya ya uwekezaji nchini
inayolenga kuweka mazingira bora ya uwekezaji,”alisema Waziri Kairuki
Amesema,
changamoto ambazo wawekezaji wamekuwa wakikabiliana nazo zinaendelea
kutatuliwa ikiwa ni pamoja na; utitiri wa kodi, ukosefu wa maji ya
uhakika, ubovu wa miundombinu ya barabara, gharamza kubwa za uzalishaji,
uzalishaji duni kwa ubora na wingi wa zabibu, ukosefu wa aina
mabalimbali za zabibu.
Changamoto
nyingine walizobainisha ni; ugumu wa kuanzisha viwanda vidogo vya
kusindika zabibu, ukosefu wa utaalamu katika kilimo cha zabibu, pamoja
na uwepo wa bidhaa zisizo na ubora sokoni.
Akijibu
changamoto hizo, Waziri Kairuki aliwatoa hofu kwa kuainisha maeneo
muhimu yaliyofanyiwa maboresho ikiwa ni pamoja na kufutwa kwa tozo na
kodi zaidi ya 168 nchini, kuendelea kuboresha miundombinu muhimu ikiwemo
barabara zinazosimamiwa na TARURA, kuwa na uhakika wa upatikanaji wa
umeme na maji ili kila mwekezaji na mfanyabiashara anufaike na
kuwekezaji kwake.
Aidha Ofisi ya
Waziri Mkuu Uwekezaji kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji nchini
inaendelea kuandaa mpango wa kuteua mabalozi kwa lengo la kuvutia
wawekezaji kama ilivyo katika sekta nyingine ikiwemo utalii.
“Tumeendelea na
hatua za awali za kuanzishwa kwa mpango wa kuwa na mabalozi watakao
tangaza masuala ya uwekezaji nchini, hii ni pamoja na kushirikisha
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kuona
namna ya kupata mabalozi hao watakaofikia taifa na nje ya
Nchi,”alisisitiza Waziri Kairuki
Aidha, alitumia
fursa hiyo kuwashauri wawekezaji kuvitumia vyema vyombo vya habari
katika kutoa elimu na kujitangaza ili kuendelea kuwa na soko la uhakika
kwa kuzingatia ubora wa bidhaa wanazozalisha.
Naye Mchumi Mkuu
kutoka idara ya Uwekezaji Bw. Francis Mollay, alibainisha baadhi ya
jitihada za kuhakikisha wawekezaji wananufaika na uwekezaji wao pamoja
na uwepo wa sheria na kanuni zinazobainisha namna bora ya kuboresha
mazingira yao ili kuwa na maendeleo katika sekta zote.
“Tunaendelea
kuboresha mazingira ya biashara kwa kupitia sheria na sera zinazohusiana
na kodi mbalimbali ili kutatua changamoto za kikodi zilizopo,”alieleza
Mollay.
Kwa upande wake
Mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza mvinyo cha Alko Vintages Bw. Archard
Kato alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendelea
kuboresha mazingira ya wawekezaji na kutoa rai kwa vijana kutumia fursa
zilizopo katika kilimo hasa cha zabibu kwa kuonesha nia na uthubuti ili
kujikwamua kiuchumi na kuondokana na changamoto ya ukosefu wa ajira.
“Vijana lazima
mjiamini na kuwa na uthubutu katika kuanzisha biashara ili kuingia
kwenye sekta ya uwekezaji, hakikisha una maono au jambo linalokuvutia na
weka mikakati ya kulifikia.Hakikisha unajaribu wazo ulilonalo na
kuwatumia walioweza katika hilo, utayaona manufaa kama kijana,”alisema
Kato.
Kiwanda kingine
alichotembelea ni Alko Vintages Co. Ltd kinachozalisha mvinyo wa aina
mbalimbali ikiwemo Dompo, Altar, St. Mary’s, Image, Rose na Klymax
viliyopo katika Wilaya ya Dodoma Mjini mkoani Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...