Na Amiri kilagalila,Njombe


Wakazi wa mitaa ya Sido na Buguruni halmashauri ya mji wa Njombe wameshindwa kuzuia hisia zao baada ya kukamilika ujenzi na kuzinduliwa kwa zahanati ya mitaa hiyo ambayo ujenzi ujenzi wake umesuasua kwa zaidi ya miaka 9.

Ujenzi huo ulioghalimu zaidi ya Mil 110 umechukua muda mrefu kukamilika kutokana na sababu mbalimbali matumizi mabaya ya fedha za ujenzi huku pia tofauti za kiitikadi zikitajwa kuwa kikwazo kikubwa katika eneo hilo.

Baadhi ya akina mama walioshiriki uzinduzi wa zahanati hiyo akiwemo Riziki Chapile na Lustika Mtundu wanasema licha ya kuwa ndani ya halmashauri ya mji lakini wamekuwa wakipata shida kufuata huduma za matibabu nje ya mitaa yao katika kituo cha afya cha Njombe Mjini na hospitali ya wilaya Kibena hali ambayo imekuwa ikihatarisha maisha ya wajawazito nyakati za usiku.

Afisa mtendaji wa mtaa wa Sido Clara Mpete katika taarifa ya ujenzi wa zahanati hiyo amesema imejengwa kwa michango mbali mbali ikiwemo ya wananchi kwa zaidi ya shilingi milioni 50,mchango wa  Mbunge,Madiwani na Serikali hadi kukamilika kwake imetumia zaidi ya Shilingi milioni 100

“Jengo hili limeghalimu jumla ya shilingi milioni mia moja na kumi na saba elfu na mia tatu,lakini kwa sasa shughuli zilizobakia ni pamoja na ujenzi wa uzio katika shimo la taka ngumu”alisema Clara

Katibu wa Afya mkoa wa Njombe Frank Mhilu anasema kuwa kukamilika kwa zahanati hiyo kunafanya mkoa kufikisha zahanati zaidi ya 240 ambazo zinakwenda kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya kwa kiasi kikubwa.

“Serikali haijaishia hapo kuwasaidia wananchi,imetoa shilingi zaidi ya bioni saba kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa ipo kule Mgodechi,na jumla ya zahanati 243 lakini leo baada ya uzinduzi wa zahanari hii tumeingiza zahanati ya 244”alisema Frank Mhilu

Dokta Isaya Mwasubila ni mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe anasema zahanati hiyo imeanza kutoa huduma zote za msingi katika ngazi ya zahanati huku zoezi la ukamilisha kwa hatua
nyingine likiendelea.

“Hapa pia tutazalisha akina mama,huduma ya maabara ipo,ya chanjo ipo,huduma za virusi vya ukimwai pia iko hapa”alisema Mwasubila .Akizindua zahanati hiyo Mbunge wa jimbo la Njombe mjini Edward Frans Mwalongo anasema kuwa katika sekta ya afya jimbo lake limekosekana zahanati katika vijiji takribani vitatu pekee kati ya vijiji 44.

“Tutafika mahala halmashauri ya mji wa Njombe tutakuwa na zahanati kila kijiji kwasababu sasa hivi tumebakiza karibu na vijiji vitatu na vyote vipo kwenye hatua mbali mbali,lakini zahanati hii imechelewa kukamilika ila kwa maana ya huduma ni daraja la kwanza”alisema Mwalongo.
Kulia ni mbunge wa jimbo la Njombe mjini Edward Mwalongo na kushoto ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Iluminata Mwenda wakisoma maelezo ya jiwe la msingi mara baada ya uzinduzi wa zahanati ya mtaa wa Matalawe na Buguruni.

Mbunge wa jimbo la Njombe mjini Edward Mwalongo akiwaomba wananchi wa mitaa miwili ya Buguruni na Matalawe kuwatunza wataalamu na wahudumu wa afya waliofikishwa katika zahanati mpya ya mitaa hiyo aliyoizindua na kuanza kutumika.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Iluminata Mwenda katikati akiwapongeza wenyeviti wa mitaa ya Buguruni na Matalawe kwa kusimamia vema na kuhakikisha zahanati ya mitaa hiyo inaanza kufanya kazi ili kusogeza huduma kwa wananchi.
Dokta Isaya Mwasubila ni mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe akifafanua huduma zinazotolewa katika zahanati mpya ya mitaa ya Buguruni na Matalawe,huku akihamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya CHF iliyoboreshwa.
 Wananchi waliofika katika uzinduzi wa zahanati wakionyesha furaha mara baada ya kuanza kutolewa kwa huduma katika zahanati yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...