
Kijana huyo amejikuta katika wakati mgumu baada ya wanakijiji kukamilisha mazishi ya mama yake mzazi ambapo mwenyekiti wa kijiji cha Wenda Denis Mpogole akaamuru familia ya bwana Damiani na mkewe kuchapwa viboko mbele ya waombolezaji kutokana na tabia yao mbaya ya kutoshirikiana na jamii kwenye matukio mbalimbali kama vile misiba.
"Wananchi wa kitongoji C Damiani inatakiwa apigwe fimbo hapa yeye na mke wake,watu wote hawa wamekuja kwasababu wanaheshimu mazishi”alisema Denis Mpogole
Licha ya kuagiza kupewa adhabu ya viboko familia ya bwana Damian mwenyekiti wa kijiji Bwana Mpogole akatoa agizo kwa viongozi wa vitongoji kuhakikisha wana anza kuwa adhibu wananchi ambao watakuwa wakisusia kushiriki katika matukio ya kijamii kwani kufanya hivyo ni kosa na utamaduni wa mwafrica hususani Mtanzania.
“Sasa sheria inasema hivi tutakapo kuta unauza biashara yeyote wakati maiti inapita pale au umeskia msiba naomba tuandikane majina bora nionekane mnafiki kwasababu toka ninavogombea nilionekana mnafiki kipaumbele”alisema Mpogole
Aidha amesema mbinu mbadala za watu kuhudhulia misibani zimetengenezwa na zitaendelea ili kufanya jitihada za kijiji hicho kuheshimika.
Nae diwani wa kata ya Mwangata Edward Nguvu Chengula akiwa katika mazishi akasema utaratibu wa kuchapa viboko utarejesha mahusiano katika jamii hivyo anaunga mkono utaratibu huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...