Yassir Simba, Michuzi TV
Mchezo wa kupashapasha misuli kabla ya kurejea kwa ligi kuu Tanzania bara VPL June 13, 2020 baina ya waoka mikate Azam Fc dhidi ya Kino Boys KMC uliopigwa jana June 10,2020 katika dimba la Azam Complex Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam umeshuhudia Azam Fc na KMC Fc wakitoka sare ya kufunguna bao moja kwa moja
Mabao ya Sergie Tape dakika ya 54 na bao la la kusawazisha kwa upande Azam Fc dakika ya 80 ya mchezo lilofungwa na kiungo Mzanzibar Mudathir Yahya Abbas mara baada ya golikipa wa KMC Juma Kaseja na mabeki zake kuchezea shillingi Chooni na kuwaruhusu Azam kupata bao la kusawazisha.
KMC wanaonekana kuimarika siku hadi siku katika michezo yao mitatu waliocheza ambapo mchezo wao wa kwanza wa kirafiki waliwacharaza bakora 3 kwa bila Yanga huku mchezo wao pili walifungwa na Simba Sc mabao 3 kwa 1 na mchezo wao wa tatu wa jana wakatoa sare ya 1-1 dhidi ya Azam Fc.
Swali ni je KMC wataendelea na moto huo katika michezo yake iliyosalia ya VPL.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...