Na Vero Ignatus.

Diwani aliyemaliza muda wake wa kata ya Tumbi wilayani Kibaha mkoa wa Pwani  Hemed Mnkai Chanyika akiwasilisha taarifa ya utekelezaji  ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020 ameeleza kuwa katika kipindi chake cha uongozi amefanikiwa kutatua changamoto mbalimbali za wananchi ikiwemo miundombinu ,elimu,Afya,maji
michezo na ardhi. 

Ameeleza hayo Jana Kibaha  kuwa katika kusimamia tatizo la ajira kwa vijana aliweza kutoa mikopo mbalimbali kwa vijana,ili waweze kujiajiri na hivyo kutokomeza tatizo hilo kwa vijana kwa kata hiyo,hadi anamaliza muda wake jumla ya vikundi zaidi ya 20 vimenufaika.

Hemed alisema kuwa kwa upande wa suala la Elimu wameweza kujenga bweni la wavulana shule ya sekondari Mwanalugali, ambalo tayari limekamilika,pamoja na kuibadilisha shule ya msingi mkoani kuwa katika mchepuo wa kingereza,imeshaanza na inaendelea vizuri.  

''Tumeweza kujenga bweni la wanafunzi katika shule ya Mwanalugali sekondari iliyopo Mwanalugali B,Ujenzi wa maabara ya kisasa katika shule hiyo,manunuzi ya vifaa vya maabara pamoja na chumba kimoja cha darasa katika shule ya msingi Mwanalugali,ujenzi wa maktaba ya shule ya msingi mwanalugali A (mchango wa wananchi na serikali)tuliweza kuongoza katika mtihani wa Taifa kwa kupata mwanafunzi kutoka Tumbi sekondari aliyeongoza kitaifa .Alisema Hemed Mnkai

Katika suala la Afya wamefanikiwa kuboresha hospital kwa kuwa na chumba cha upasuaji ili kupunguza au kuondoa kabisa vifo vya mama na watoto katika hospital zilizopo ndani ya kata ya Tumbi,Kwa kutumia fedha za ndani za mfuko wa jimbo.

Alisema kuwa wamefanikiwa kununua majenereta kwajili ya kituo cha afya mkoani chumba cha upasuaji kina mama,duka la dawa la jamii ,upanuzi wa hospitali ya mkoa ya Tumbi,ambapo waliishawishi serikali kuleta fedha ili kukidhi mahitaji ya hospital hiyo ya Rufaa(Tumbi)

''Kujenga hospitali ilikuwa kilio kikuu cha kwa wana Bokomnemela na Bokotimiza na sasa imekamilika kwa asilimia 90% ,wakati tunaandika andiko hili ,hata hivyo tumetenga 50m ili kuikamilisha kabla ya oktoba 2020 ili ianze kutumiwa na kuondoa adha maeneo hayo na maeneo jirani ''Alisema Diwani huyo aliyemaliza muda wake.

Aidha alisema  wameweza kutatua migogoro ya ardhi muliodumu kwa miaka mingi block (E)Mwanalugali A+B ambapo walifanikiwa kuwarejeshea wananchi katika viwanja vyao,sambamba na kugawa mbegu za mikorosho na kuhamasisha wakulima mmoja mmoja na vikundi kuchangamkia matrekta ambayo yanakopeshwa na NDC Tamko Kibaha kupitia tamko la mh.Mgufuli kuwawezesha wananchi kupata matrekta na kuondokana na jembe la mkono.

''Naweka msisitizo kuhakikisha kuwalipa fidia kwa ambao bado wanadai kufidiwa ,ili kuweza kupisha miundombinu mingine kupitia maeneo hayo yenye utata''

Aidha Katika kushughulikia masuala ya miundo mbinu katika kata ya Tumbi walihakikisha wamechonga barabara ikiwemo KEC-Bokotimiza Tanesco -Mwanalugali(Shule ya mkoani-Mwanalugahali )barabaraya magereza na ile ya mizani-whipaz,pia wameweza kujenga barabra kwa kiwango cha changarawe,sambamba na barabara za lami Tughe Anglican mkoani A,pamoja na barabara ya magereza ,Nida mpaka kwa mkuu wa wilaya.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya siasa wilaya Bi  Zamda Komba alisema kuwa maendeleo hayawezi kuletwa na mtu mmoja bali yanaletwa kwa ushirikiano hivyo wananchi wanapaswa kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi ili kiendelee kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Komba alisema kuwa Wanaccm wanapaswa kuunga mkono wagombea wa chama na kuacha kuwahujumu wagombea wao kwani kuna baadhi ya wanachama wamekuwa wakikihujumu chama jambo ambalo linasababisha kushindwa kwenye baadhi ya chaguzi. 
 Picha Diwani aliyemaliza muda wake kata ya Tumbi wilayani Kibaha mkoa wa Pwani  Hemed Mnkai Chanyika 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...