WATUMUSHI wawili wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka manne yakiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka na kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali Ipyana Mwakatobe leo Juni 17, 2020 imewataja washtakiwa hao kuwa ni, Peter Mrema na Adam Yusuf ambao ni waajiriwa wa wizara kama wathamini wa ardhi katika ofisi ya Mthamini Mkuu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Kassian Matembele imedaiwa, Juni 20, 2016 katika Ofisi za Mthamini Mkuu wa Serikali Wilayani  Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Yusuf akiwa kama mthamini wa wizara hiyo, wakati wa utekelezaji wa kazi yake kwa makusudi alipitisha ripoti ya uthamini kwa ajili ya malipo ya fidia katika mradi wa Dar Metropolitan Development (DMDP) na kumsababishia mshtakiwa mwenzake Mrema faida ya zaidi ya Sh milioni 46.6.

Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa Yusuf akiwa na lengo kumdanganya mwajiri wake kwa makusudi alitumia taarifa iliyotolewa Aprili, 2016 yenye taarifa za udanganyifu ikiwa na orodha ya majina na thamani ya viwanja kwa ajili ya fidia katika mradi huo wakati akijua taarifa hizo ni za uongo na anamdanganya mwajiri wake.

Pia mshtakiwa Mrema anadaiwa kuwa siku na mahali hapo alitumia taarifa ya udanganyifu iliyotolewa June, 2014 kumdanganya mwajiri wake. 

Katika shtaka la nne imedaiwa, kati ya Juni 1, 2014 na Aprili 30, 2016 jijini Dar es Salaam mshtakiwa Mrema, alijifanya mtathmini kwa kuandaa taarifa ya utathmini wa ardhi bila usajili inayoonesha kuwa ilitolewa kati ya June, 2014 na April, 2016 kwa manispaa ya Ilala na Temeke huku akijua hana usajili wa kazi hiyo.

Hata hivyo washtakiwa hao wamekana mashtaka hayo na wako nje kwa dhamana .Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Julai Mosi, 2020.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...