Na.
Frank Mvungi na Immaculate Makilika - MAELEZO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la
msingi la mradi wa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami katika mji wa Serikali
utakaogharimu zaidi ya bilioni 89 ikiwa ni ahadi aliyotoa mara baada ya
kutangaza Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi ili kutekeleza tamko alilolitoa Baba
wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1973 zaidi ya miongo mine iliyopita.
Akizungumza
leo Jijini Dodoma wakati akiweka jiwe la msingi la mradi huo na baadae kuzindua
jengo la Ofisi za Wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA) alisema wakala
huo umetekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuwataka kuongeza kasi zaidi.
“Ujenzi
wa barabara hii utakua na njia nne zenye urefu wa km 11.2, njia mbili zenye
urefu wa km 28, njia za waenda kwa miguu, njia za baiskeli na limetengwa eneo
la huduma za kijamii,”
“Dodoma
ni mji unaokua vizuri, kuna miradi mikubwa iliyokwishatekelezwa na inayotarajiwa
kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa barabara ya mzunguko ya njia nne yenye urefu wa
km 110 itakayogharimu zaidi ya shilingi bilioni 600 na ujenzi wa Uwanja wa
Ndege mkubwa utakaogharimu shilingi bilioni 500” alisisitiza Rais Dkt. Magufuli.
Aidha,
Rais Magufuli alitoa tahadhari kwa TARURA kutumia fedha zilizotengwa kwa ajili
ya ujenzi wa barabara na sio kuendelea kujenga ofisi zingine katika wilaya
mbalimbali nchini na badala yake watumie majengo ya Serikali katika mikoa na
wailaya mbalimbali nchini.
Vilevile,
Taasisi za Serikali zimetakiwa kujenga majengo yake badala ya kuendelea kulipa
pango katika majengo ya kukodi, na ameitaka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)
kumaliza ujenzi wa jengo lake hapa
jijini Dodoma kabla ya mwaka 2020 kumalizika.
Aidha,
Rais Magufuli alisema kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Fedha Duniani (IMF)
imeidhinisha dola za Marekani milioni 14.3 za msamaha wa kodi ya madeni ambayo
nchi ilikuwa ikidaiwa na kutaja sababu ya msamaha huo kuwa nchi imefanikiwa kupambana
vizuri dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu (Covid-19) unaosababishwa na
virusi vya Corona.
“Kwa
niaba ya watanzania nitamuandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa IMF kumpongeza
kwa kutambua juhudi zetu na fedha hizi tutazitumia vizuri katika kupambana na ugonjwa
huu pamoja na kushughulikia mambo mengine yakayosaidia ugonjwa huu usije tena”
alisisitiza Rais Magufuli
Wakati huo huo, Rais Magufuli amekabidhi
pikipiki kwa Maafisa Tarafa kwa lengo la kutatua changamoto ya usafiri iliyokuwa
ikiwakwamisha katika kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali katika maeneo
yao.
“Nilitoa
kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kununua pikipiki hizi, zimepatikana
pikipiki 448 na Maafisa Tarafa ni 570 nchi nzima, hivyo natumaini hakuna
Ofisa Tarafa atakayekuwa hana pikipiki kwani kuna waliogawiwa zamani, watakaoharibu
ama kupoteza watazilipa” alisisitiza Rais Magufuli.
Akizungumzia
kuhusu ugonjwa wa corona, Rais Magufuli ameitaka Wizara ya Afya kukiendeleza Kitengo
cha Tiba Asili kuendelezwa sambamba na kuongeza bajeti yake, na kuwataka
wanaotengeneza dawa za asili kutodharauliwa.
“Corona
bado haijaisha lakini imepungua sana, hivyo tuendelee kuchukua tahadhari, watu
waliodhani tutafariki wengi wameshindwa. Mungu wetu anatupenda na tuendelee
kumtegemea yeye” aliongeza Rais Magufuli.
Katika hatua
nyingine, Rais
Magufuli wakati wa ufunguzi wa jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji amesema kuwa moja ya changamoto zilizokuwa zikilikabili Jeshi hilo ni
upandishwaji wa vyeo kwani waliokuwa juu hawakujali wa chini, hali
iliyosababisha tuchukue hatua kwa kuwapandisha vyeo Makamanda 889.
Tunawahakikishia tutaendelea kuwapandisha kadri itakavyowezekana.
Akizungumzia
utendaji wa Jeshi hilo, Rais Magufuli amesema kuwa ameshatoa maagizo kwa
Taasisi ya Nyumbu kushirikiana na Jeshi
hili kuanza kutengeneza magari ya zimamoto nchini.
“Kulikuwa
na mapendekezo ya Makamishna wanne wa jeshi hili kushushwa vyeo au kufukuzwa
kazi lakini kwa kuwa mmefanya marekebisho ya kutosha nimewasamehe, hata
aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi, Thobias Andengenye nimemsamehe lakini
nitampangia kazi nyingine,”alisisitiza Rais Magufuli.
Aidha,
ametoa wito kwa Viongozi wa Manispaa, Majiji na Wizara ya Ardhi kuhakikisha wanawaelimisha
watu kuwa katika kila jengo itengenezwe njia zitakazotumiwa na jeshi hili mara
yanapotokea majanga ya moto.
Kwa
kutambua umuhimu wa jeshi Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Rais ameahidi kuwaunga
mkono kwa kuwapa shilingi bilioni 5 ndani ya wiki hii ili kutatua changamoto ya
makazi ikizingatiwa tayari jeshi hilo limetafuta eneo la kujenga makazi ya
familia 80.
Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga alimshukuru Rais Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kuwapa kiasi cha shilingi bilioni 2,656,146,300 kwa ajili ya
ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dodoma.
Aidha,
Jeshi hilo limepata mafanikio katika
kukabiliana na matukio ya moto 6,398 na maokozi 2,663 yalishughulikiwa kuanzia
mwaka 2015/2016 hadi 2019/2020 ambapo maeneo 319,389 na vyombo vya moto 17,740
vimekaguliwa ili kuimarisha hali ya usalama wa wananchi na mali zao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo
wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi mradi wa ujenzi wa Barabara
za lami zenye jumla ya km 51.2 katika mji wa Serikali (Mtumba) mkoani Dodoma
leo tarehe 11 Juni 2020.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...