Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.
Innocent Bashugwa akikagua bidhaa ya unga wa viazi lishe unaochakatwa
na mashine kutoka SIDO na kampuni Ng’hami Industries Company Ltd iliyopo
Maswa – Simiyu. Leo 30 juni 2020
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.
Innocent Bashugwa akipokea maelekezo ya mchato mzima wa uandaaji wa
viazi lishe jinsi vivyochakatwa hadi kupata unga wa viazi lishe katika
kiwanda cha Ng’hami Industries Company Ltd kilichopo Maswa – Simiyu. Leo
30 juni 2020
(Picha zote na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara)
…………………………………………………………………………………….
Na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara
Waziri wa Viwanda
na Biashara Mhe Innocent Bashungwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwafukuza kazi wafanyakazi wa shirika
hilo wanaowatoza fedha na wanaochelewesha zoezi Kutoa nembo ya ubora
kwa bidhaa zinazotengenezwa kwenye Viwanda vidogo nchini.
Waziri
Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo 30 juni 2020 alipofanya ziara
mkoani Simiyu na kutembelea kiwanda cha Usindikani wa Viazi lishe
kilichopo wilaya ya Maswa kinachojulikana kwa jina la Ng’hami Industries
Company Ltd.
Bashungwa
amefikia maamuzi hayo baada ya kufika kiwandani hapo na kukagua bidhaa
za kiwanda hicho ambayo ni unga wa viazi lishe na kugundua hazina nembo
ya ubora ya TBS, ambayo changamoto hiyo imesababiswa na wafanyakazi wa
shirika la TBS kwa kuwaomba fedha kwa ajiri ya kupewa nembo ya ubora pia
kuchewesha kwa zaidi ya miezi saba bila kupewa majibu au nembo ya
ubora.
Waziri
Bashungwa baada ya kuona changamoto hiyo alimpigia simu Mkurugenzi Mkuu
wa TBS na DKt. Yusuph Ngenya na kumuelekeza kuwafukuza kazi wafanyakazi
wake wanaokwenda kinyume na maagizo ambayo amekuwa akiyatoa mara kwa
mara ya kutowachelewesha wafanyabiasha kwa sababu ambazo sio za msingi
zinazosababisha bidhaa kutopewa nembo za ubora kwa wakati ambazo
zinasababisha mazingira ya Rushwa na usumbufu kwa wazalishaji wa bidhaa
mbalimbali.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bw. Ntobi Rufunga ameeleza kuwa
barua ya kuomba nembo ya ubora ilipelekwa TBS tangu mwezi 11, 2019
lakini mpaka sasa hajapewa majibu yoyote na baada ya kuchukuliwa kwa
sampuli ya bidhaa hiyo wameombwa kutoa kiasi cha Tsh. 520,000/= ili
wapewe nembo ya ubora ambayo ni kinyume na sheria na mashariti ya
shirika hilo.
Aidha Bw.
Ntobi amesema kuwa Kiwanda hicho mpaka sasa kinazalisha unga wa viazi
lishe wa aina mbili ambao ni Unga wa kupika uji kwa ajiri ya matumizi ya
rika zote pia Unga wa kutengeneza keki, mikate na andazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...