Na Eliud
Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara.
Waziri
wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa amezielekeza FCC, EWURA, WMA
kufanya ukaguzi na kuwachukulia hatua wafanyabiashara na waagizaji wa mafuta
wanaoficha bidhaa hiyo kwa lengo la kuyauza kwa bei ya juu yatakapoadimika au
kupanda bei.
Waziri
Bashungwa aliyasema Juni 17, 2020 jijini Dar es salaam katika kikao kazi na
Watendaji wa Mamlaka za Tume ya Ushindani (FCC), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati
na Maji (EWURA), Wakala wa Vipimo (WMA), Mamlaka ya Bandari (TPA) pamoja na TRA
kwa lengo la kufanya mapitio na marekebisho ya utaratibu wa kanuni ya bei
elekezi ya mafuta kwa bidhaa za petroli zinazoingizwa nchini kupitia bandari za
Dar es Salaam, Mtwara na Tanga, kwa nia ya kuwezesha manufaa ya punguzo la bei
kuwafikia wananchi sa mikoa yote nchini kwa usawa.
‘‘Katika kipindi cha mapambano ya Covid-19, moja ya
fursa tulizozipata kama nchi ambayo pia tulipata maambukizi ni kushuka kwa bei
ya mafuta, na sisi kwa sababu tunaingiza mafuta kutoka nje ya nchi, kushuka kwa
bei ya mafuta duniani sisi tumenufaika lakini pamoja na kunufaika huku kwa
kushuka kwa bei ya mafuta kuna baadhi ya mikoa bado bei ipo juu”
Aidha, Bashungwa ametoa onyo kali kwa
wafanyabiashara wote ambao bado wana tabia za kuficha bidhaa mbalimbali pindi
zinaposhuka bei au kuadimika kwa lengo la kujipatia kipato kikubwa, ameielekeza
taasisi ya Tume ya Ushindani na Ewura kufanya msako mkali kama ulifanywa kwenye
sukari ili kuwabaini na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wote wanaoendeleza
tabia hizo
"Wafanyabiashara tunajua bei ambazo
wananunulia mafuta na kipindi cha COVID-19, mfanyabiashara yoyote ambaye
amenunua mafuta kwa bei ya punguzo lakini punguzo hilo halijaenda moja kwa moja
kwa mlaji kwa maana ya mwananchi maeneo yote nchini ambayo wafanyabiashara hawa
wanaingiza mafuta na kusambaza, tutatumia taasisi zetu ya Tume ya Ushindani na
Ewura kuhakikisha kote nchini tunafatilia na kama kuna mfanyabiashara yoyote wa
mafuta ambaye ana hodhi mafuta ili kupata faida tutatumia sheria kumchukukulia
hatua kali kama tulivyofanya kwenye sukari,"
Waziri
Bashungwa amesisitiza kuwa kuwa mapendekezo ya wataalamu katika kikao kazi
hicho yatapelekwa kwa Waziri mwenye dhamana ya Nishati na Madini baada ya
kukamilika leo hii ili kumshauri kuhusu namna ya kuweka uwiano sawa wa bei
elekezi kwa bidhaa husika, huku akisisitiza kuwa wafanyabiashara watakaobainika
kukiuka taratibu za leseni walizopatiwa na EWURA na wanaokiuka kanuni, sheria
na taratibu za Ushindani watachukuliwa hatua za kisheria, ikiwamo kunyang'anywa
leseni za kufanya biashara ya bidhaa za petrol
Awali,
Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA),
Mhandisi Godfrey Chibulunje amesema kuwa “Mafuta yanayouzwa nchini yanapokelewa
kupitia bandari za Dar es salaam, Tanga na Mtwara. Katika kukokotoa bei ya
mafuta, mikoa ya Kaskazinini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara) hupangiwa
bei zao kulingana na gharama ya mafuta yanayopokelewa kupitia bandari ya Tanga.
Mikoa ya kusini (Mtwara, Lindi na Ruvuma) hupangiwa bei kulingana na gharamaya
mafuta yanayopokelewa kupitia bandari ya Mtwara. Mikoa mingine yote hupangiwa
bei zao kulingana na gharama ya mafuta yaliyopokelewa kupitia bandari ya Dar es
salaam.
Sambamba
na hayo Mhandisi Godfrey amesoma mapendekezo ambayo yataleta mabadiliko ya
kanuni za kukokotoa bei za mafuta ambayo ni;
Kuweka
usawa wa premium kwa bandari zote na hivyo kuwa na bei za mafuta zenye
ushindani na watumiaji wa mafuta kununua kwa bei ambayo ina usawa, kuweka
kanuni za kubadilisha gharama za mafuta kila mwezi kulingana na mabadiliko ya
soko la dunia, kuendelea kuwepo kwa nafasi ya ushiriki wa kampuni za wazawa
katika zabuni za BPS.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa akitoa ufafanuzi na maelekezo kuhusu bei ya mafuta kwa bidhaa ya petroli katika kikao kazi kilichowakutanisha Watendaji wa Mamlaka za Tume ya Ushindani (FCC), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Wakala wa Vipimo (WMA), Mamlaka ya Bandari (TPA) pamoja na TRA. 17 juni 2020 jijini Dar es salaam (Picha na Eliud Rwechungura - Wizara ya Viwanda na Biashara)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...