Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya I&M, Bw. Baseer Mohammed (wa pili kulia) akizungumza mbele ya Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Abel Makubi wakati akikabidhi msaada wa matanki maalum ya kuoshea mikono (handwashing tanks) pampja na sabuni zake kwa Wizara ya Afya vyenye thamani ya Sh10 milioni. Wakisikiliza kulia ni Mkuu wa Idara ya Wateja wa rejareja wa Benki ya I&M, Bi Lilian Mtali na kushoto Bi Angelina Ngalula Mwenyekiti TPSF.
Mkuu wa Idara ya wateja wa rejareja wa benki ya I&M, Lilian Mtali akionyesha mfano wa matumizi ya tanki maalum la kuoshea mikono (handwashing tank) mara baada ya benki hiyo kukabidhi matanki makubwa matano pamoja na sabuni vyenye thamani ya Sh10 milioni kwa Wizara ya Afya katika jitihada za kuendelea kuhamasisha jamii kunawa mikono mara kwa mara ili kujiepusha na magonjwa yatokanayo na uchafu wa mikono.
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Abeli Makubi (wa pili kushoto), Mkuu wa Idara ya wateja wa rejareja wa benki ya I&M, Lilian Mtali (wa tatu kushoto), akifuatiwa, Bi. Anitha Pallangyo, meneja masoko na mawasiliano wa benki ya I&M, mara baada ya benki hiyo kukabidhi msaada wa matenki maalum ya kuoshea mikono kwa wizara ya Afya yatakayotumika kusaidia jamii kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...