Benki ya NMB imekabidhi vifaa vyenye thamani ya
Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Makambini
Halmashauri ya Mji wa Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe kusaidia kukabiliana
na janga la ugonjwa hatari wa COVID-19.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kwa niaba ya Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Meneja wa NMB Tawi la Mbalizi Road - Hamadan Silliah amesema msaada wa vifaa hivyo ni moja kati ya mpango wa NMB ya kutenga sehemu ya faida yake katika kusaidia huduma za kijamii.
Silliah amesema kuwa Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu ilipokea maombi ya kusaidia ujenzi wa kituo hicho na kwamba moja kati ya sera za NMB kurejesha faida katika huduma za kijamii ni pamoja na kusaidia katika kukabiliana na majanga na huduma za Afya.
Amesema kutanuka kwa huduma za Benki hiyo kumeongeza pia uwepo wa huduma za NMB mkononi kupitia simu za kiganjani na hii imesaidia kufanya muamala kwa njia za Kidijitali ikiwa ni moja ya sehemu ya kujikinga na ugonjwa wa CORONA.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Tunduma Bi. Regina Bieda amesema ujenzi wa kituo hicho kinachotarajiwa kuwa na wodi mbili za akina mama na wanaume kinatarajia kugharimu kiasi cha Sh.Milioni 95 hadi kukamilika kwake.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya ya Momba Juma Said Irando amesema kuwa Benki ya NMB imekuwa na mchango mkubwa katika huduma za kijamii na kuwa msaada katika kituo hicho cha Afya ni Mahsusi kwa magonjwa ya milipuko.
Amesema kituo hicho kipo mpakani ambayo ni njia kuu kuelekea nchi za SADC hivyo kumekuwa na muingiliano wa wageni kutoka nchi zilizopo kusini na DRC Kongo na kuwa awali kituo hicho kilitengwa kwa ajili ya EBOLA na sasa kinaboreshwa kutokana na ugonjwa hatari wa COVID-19.

Mkuu wa Wilaya ya Momba - Juma Said Irando (wapili kushoto) akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa vifaa vya ujenzi ikiwemo nondo, mbao za kenchi na mifuko 171 ya saruji. Wakwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu - Hamadan Silliah.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...