Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka (kulia), akizungumza jambo baada ya kutangazwa kuunganishwa kwa Benki ya TIB na TPB Corporate, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dodoma.

 Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka, akiwahakikishia wateja wa Benki ya TIB na TPB kuwa huduma hazitaathirika kutokana na kuunganishwa kwa Benki hizo, wakati wa Mkutano na vyombo vya Habari, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dodoma.

 

 Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka, wa tatu kushoto na   Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi baada ya  kutangazwa kuunganishwa kwa Benki ya TIB na TPB Corporate, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dodoma.



Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka (kulia), akisikiliza jambo baada ya kutangazwa kuunganishwa kwa Benki ya TIB na TPB Corporate, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dodoma.

Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka (wa pili kulia), wakiangalia baadhi ya nyaraka zinazohusu kuunganishwa kwa Benki ya TIB na TPB Corporate, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dodoma. (Picha na Ramadhani Kissimba, WFM, Dodoma)

Na Ramadhani Kissimba 
na Peter Haule, WFM, Dodoma

Serikali imeamua kuziunganisha Benki ya TPB na TIB Corprate kuanzia Juni Mosi, 2020 kwa lengo la kuboresha utendaji wa benki inazomiliki ili kuwa na Benki moja ya biashara ambayo ni imara.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Msajili wa Hazina, Bw. Athumani Mbuttuka, katika Mkutano na Waandishi wa Habari.

Bw. Mbuttuka alisema kuwa muungano wa Benki hizo unalenga kuleta mageuzi makubwa ya kiutendaji, kimfumo, kimuundo na taswira ili benki hiyo iweze kuhimili ushindani wa kibiashara kwenye sekta ya fedha.

“Serikali inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kuhakikisha utendaji wa benki zake unaimarika na maslahi ya wenye amana na wateja wote yanalindwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa Benki na taasisi za fedha”, alieleza Bw. Mbuttuka

Bw. Mbuttuka alisema kuwa kwa hatua ya awali, Benki ya TPB itachukua mali na madeni ya Benki ya TIB Corprate na Wateja wote wa Benki ya TPB na Benki ya TIB Corporate wataendelea kuhudumiwa kwenye matawi yao ya sasa hadi hapo watakapotaarifiwa vinginevyo.

Aidha alisema kuwa Serikali inawahakikishia wateja wa benki hizo mbili pamoja na umma kuwa huduma za kibenki hazitaathirika kwa vyovyote vile kutokana na mabadiliko hayo

Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali zenye lengo la kuboresha utendaji wa mashirika na taasisi za umma ikiwemo kuunganisha taasisi zinazotekeleza majukumu yanayofanana, ili kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...