
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Dk. Edmund Mndolwa,(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa tarifa ya kupata faida ya kodi ya Sh.bilioni 15.9 kwa mwaka Desemba 2019.Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Mushingi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi,(kulia) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa kutoa tarifa ya kupata faida ya kodi ya Sh.bilioni 15.9, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki ya TPB, Dkt. Edmond Mndolwa.

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa benki hio wakibadilishana mawazo katika mkutano mkuu wa 28 wa wanahisa wa Benki hiyo ya TPB wakati wa kutolewa taarifa ya kupata faida ya kodi ya shilingi bilioni 15.9 kwa mwaka Desemba mwaka 2019.
Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB Dk.Edmund Mndolwa amesema benki hiyo imepata faida ya baada ya kodi ya Sh.bilioni 15.9 kwa mwaka unaoishia 31 Desemba mwaka 2019.
Akuzungumza leo Juni 7,2020 wakati wa Mkutano wa 28 wa Wanahisa wa benki hiyo Dk.Mndolwa amewaambia waandishi wa habari kuwa Benki ya TPB imeendelea kuimarika kwa kutengeneza faida kubwa hadi kufikia faida kabla ya kodi ya Shilingi bilioni 23.0.
"Mafanikio haya yaliyopatikana kwa mwaka 2019 yanatokana na juhudi kubwa iliyofanywa na Menejimenti na wafanyakazi chini ya ushauri wa karibu wa Bodi ya Wakurugenzi katika utendaji kazi wa kila siku na kujituma kwa wafanyakazi wote kwa ujumla,"amesema.
Dkt. Mndolwa amesisitiza ingawa Benki ya TPB ina mtaji mdogo ukilinganisha na benki zingine, lakini wameweza kufanya vizuri kwa takribani miaka minne mfululizo kwenye sekta ya benki nchini na kuongeza kuwa faida nzuri iliyopatikana kwa mwaka 2019, Benki inatarajia kutoa gawio la fedha taslim kwa wanahisa wake ikiwa ni sehemu ya faida iliyopatikana.
"Hii ni kulingana na sera na taratibu ambazo Benki imejiwekea ili kuendelea kuimarisha uendeshaji wake lakini pia kugawa sehemu ya faida kwa wanahisa.Nina imani wanahisa wote watafurahia kupata gawio la fedha taslim ambapo kwa mwaka huu litaongezeka ukilinganisha mwaka uliotangulia kwa kadri Benki inavyoendelea kujiimarisha na kutengeneza faida kubwa zaidi,"amesema Dk. Mndolwa.
Amefafanua kuwa faida iliyopatikana mwaka 2019 inatajwa na uongozi wa benki kuwa ni kubwa ambayo haijawahi kufikiwa tangu kuanzishwa kwa Benki ya TPB takriban miaka 95 iliyopita.
Amesema benki hiyo itaendelea kujipanga na kupanua shughuli zake za kibenki nchini na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto za kiuchuni kwa sasa katika sekta ya fedha nchini.
"Napenda kuchukua fursa hii kuwasihi wateja wote na watanzania wote kwa ujumla pamoja na taasisi mbalimbali kuendelea kuitumia Benki ya TPB katika kuiunga mkono kwenye shughuli zake ili iweze kutimiza malengo yake vyema,"alihitimisha Dk. Mndolwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...