Aliyekuwa Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Kata ya Segerea Edwin Mwakatobe akikabidhi kadi ya CHADEMA jana 19/2020 kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma (PICHA NA HERI SHAABAN)
Wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Ilala wakifatilia kikao cha Kamati ya siasa Juni 19/2020(PICHA NA HERI SHAAABAN)
Na Heri Shaaban
CHAMA CHA Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala kimepokea waliokuwa madiwani sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)TLP na ACT katika kikao cha Halmashauri Kuu Wilaya ya Ilala .
Akipokea madiwani hao Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma alisema katika uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na madiwani chama hicho kitashinda majimbo pamoja na Kata.
Ubaya Chuma alisema Chama cha Mapinduzi CCM kimejipanga vizuri kuakikisha kinashinda kwa kishindo.
Akizungumzia kuwapokea waliokuwa madiwani wa CHADEMA alisema CCM ni nyumbani wote watarudi.
Wakati huo huo Mwenyekiti Ubaya Chuma aliwataka wana CCM kushirikiana katika kuisaidia halmashauri suala la ukusanyaji wa mapato kuakikisha halmashauri ya Ilala inavuka lengo.
Pia aliwataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Halmashauri ya Ilala wafanye kazi kwa weledi kwenda na kasi ya Rais John Magufuli ikiwemo kusimamia miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi wa kila eneo.
"Naomba Wenyeviti wa Serikali za mitaa msimamie majukumu yenu msiwe chanzo cha migogoro yenu, Mwenyekiti atakayekwenda kinyume atavuliwa madaraka yake"alisema Chuma
Akiwataja madiwani hao alisema Kassim Msham, Dorcus Rukiko, Bonaventure Mphuru Edwin Mwakatobe, Joseph Ngoa, na Joseph Saenda.
Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya Ilala Idd Mkoa aliwataka wana CCM kuchapa kazi kwa bidii kuunga mkono juhudi za Rais katika kujenga Tanzania ya Uchumi wa viwanda.
Naye aliyekuwa Diwani wa CHADEMA Kata ya Pugu Bonaventure Mphuru alisema Ilani ya CCM inatekelezwa vizuri yupo pamoja na Rais John Magufuli ,aliwataka Watanzania kumtumia Rais vizuri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...