Sehemu ya pikipiki 40 na Baiskeli
736 zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini na Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa Chama Cha Mapiduzi
ikiwa ni mchango wake wa kusaidia utendaji wa shughuli za Chama hicho
kwenye Kata na matawi mbalimbali ya jimbo hilo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mlezi wa CCM mkoa wa
Tabora, Ndugu Afadhali Taib Afadhali akikabidhi baiskeli kwa viongozi wa
matawi ya CCM jimbo la Nzega vijijini. Baiskeli 736 zimetolewa na
Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini na Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dkt. Hamisi Kigwangalla ikiwa ni mchango wake wa kusaidia utendaji wa
shughuli za Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye Kata na matawi mbalimbali
ya jimbo hilo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mlezi wa CCM mkoa wa
Tabora, Ndugu, Afadhali Taib Afadhali akikabidhi pikipiki aina ya Boxer
kwa Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ugembe jimbo la Nzega vijijini. Pikipiki
hiyo ni miongoni mwa pikipiki 40 zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la
Nzega Vijijini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla
ikiwa ni mchango wake wa kusaidia utendaji wa shughuli za Chama cha
Mapinduzi (CCM) kwenye Kata na matawi mbalimbali ya jimbo hilo.

Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini
na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifurahia na
kuonyesha alama ya ushindi wakati wa mkutano wake na wajumbe wa Mkuu wa
Jimbo la Nzega vijijini kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa
kipindi cha wamu ya tano.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wa
Jimbo la Nzega Vijijini wakifuatilia hotuba ya utekelzaji wa Ilani ya
CCM kwa kipindi cha miaka iliyokuwa ikitolewa na Mbunge wa jimbo la
Nzega Vijijini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi
Kigwangalla.

Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini
na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akieleza
utekelzaji wa Ilani ya CCM na ahadi alizozitoa kwa kipindi cha miaka
wakati wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la Nzega Vijijini

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora
Ndugu Hassan Wakasuvi akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya
Chama cha Mapinduzi alipokua akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa
CCM jimbo la Nzega Vijijini.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mlezi wa CCM mkoa wa
Tabora, Ndugu, Afadhali Taib Afadhali akizugumza jambo na Mbunge wa
jimbo la Nzega Vijijini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi
Kigwangalla ikiwa mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa jimbo la
Nzega vijijini.

Mjumbe wa Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mlezi wa CCM mkoa
wa Tabora, Ndugu, Afadhali Taib Afadhali akizugumza na wajumbe wa
mkutano mkuu wa CCM jimbo la Nzega vijijini .
PICHA/ Aron Msigwa – NZEGA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...