Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro
(Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Burundi nchini leo Jijini
Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Ndumbaro akisaini
kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Burundi nchini leo Jijini Dar es
Salaam. Kushoto kwake ni Balozi wa Burundi nchini, Mhe. Gervais Abayeho.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Burundi nchini kufuatia kifo cha Rais wa Taifa hilo Pierre Nkurunziza aliyefariki Juni 08, 2020.
Akizungumza mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi ubalozi wa Burundi nchini, Dkt. Ndumbaro ametoa pole kwa wananchi wote wa Burundi na kuwasihi kuendelea kuwa watulivu na wastahimilivu wakati huu wa msiba.
"Kusaini kitabu cha maombolezo ni ishara ya ushirikiano wetu, umoja wetu na undugu wetu na ndugu zetu wa Burundi. Kifo cha Rais Nkurunzinza kinawahusu pia watanzania kwa sababu Rais Nkurunzinza ni Rais aliyekuwa karibu sana na Tanzania kuliko nchi nyingine yeyote ile, lakini pia Burundi ipo karibu sana na Tanzania, Amesema Dkt. Ndumbaro.
Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa, Pengo la Rais Nkurunzinza ni pengo kubwa sana kwa watanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Afrika kwa ujumla.
Nae Balozi wa Burundi nchini, Mhe. Gervais Abayeho, amemshukuru Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro kwa kufika kwake kuhani msiba huo na kuongeza kuwa hali hiyo inaonesha upendo ambao unaendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya mataifa hayo mawili.
Aidha, Serikali ya Burundi kupitia ubalozi wake hapa nchini, imetoa mualiko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wa kushiriki mazishi ya Rais Nkurunzinza yanayotarajiwa kufanyika Alhamisi tarehe 18 Juni 2020 nchini Burundi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...