Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

"SIWEZI KUPUMUA" ni kauli ya mwisho ya George Floyd mmarekani mweusi aliyefariki baada ya kukandamizwa shingo kwa dakika takribani nane hadi kupoteza uhai na afisa wa polisi wa Minneapolis Derek Chauvin akituhumiwa kutoa pesa bandia ya dola ishirini katika duka moja akiwa ananunua sigara.

Floyd (46) alizaliwa Kaskazini mwa Carolina na kuishi Houston na Texas akiwa mdogo na alihamia Minneapolis miaka ya nyuma baada ya kutoka gerezani kwa lengo la kutafuta kazi (Christopher Harris, rafiki wa karibu wa Floyd ameieleza Sky News.)

Wengi walimwita 'Gentle giant' au 'Big Floyd' na hiyo ni kutokana na upendo aliouonesha kwa kila mtu aliyekutana naye hasa katika maeneo aliyowahi kufanya kazi.

Floyd alikuwa baba wa mtoto mmoja wa miaka sita anayeishi na mzazi mwenzake Roxie Washington huko Houston ambaye pia amemwelezea Floyd kuwa ni baba bora waliyeshirikiana vyema kumlea binti yao Gianna.

Big Floyd pia ameacha mchumba Courteney Ross ambaye ameeleza kusikitishwa na kuumizwa na kifo hicho.

" Aliupenda mji huu, alihama toka Houston na kuja kuishi huku kwa ajili ya watu na kutafuta fursa" amenukuliwa Ross.

Floyd aliyeelezwa kuwa mkimya wakati akisoma pia alikuwa na kipaji cha kucheza mpira wa miguu na kikapu na hakufanikiwa kumaliza shule alianza kuimba Muziki 'Hip Hop' na kundi la Screwed Up Click na baada ya kupambana na kutafuta kazi Houston akahama mji na kwenda Minneapolis ambako alipata kazi mbili; ya kuendesha malori na ulinzi katika mgahawa wa Conga Latin Bistro ambapo wateja wengi kupitia mitandao ya kijamii wameeleza upendo aliokuwa nao Floyd.

Rekodi za mahakama zinaonyesha kuwa Floyd aliwahi kushtakiwa kwa wizi wa kutumia silaha mwaka 2007 na kuhukumiwa miaka mitano jela baada ya kukiri mwaka 2009.

Katika video hiyo ya ukatili wa hali ya juu na yenye ubaguzi ilimuonesha Floyd akilalamika kwa maumivu mbele ya askari polisi aliyekuwa akimtesa kabla ya gari ya wagonjwa kumchukua na kumpeleka hospitali ambako ilielezwa amefariki dunia kwa kukosa hewa na kupata majeraha katika ubongo.

Licha ya askari aliyesababisha kifo hicho Derek Chauvin akishtakiwa kwa kosa la kumuua Floyd bila kukusudia na askari wengine watatu waliohusika wakifukuzwa kazi maandamano makubwa kuwahi kutokea yamewakusanya raia wa Marekani kutoka miji zaidi ya 20 ikiwemo Colifornia, Texas, Florida, Minnesota, Ohio na Georgia wakipinga kitendo hicho.

Marekani imeamua kutumia jeshi kutuliza vurugu za waandamanaji kwa maandamano hayo yanayoendelea nchi nzima Sasa, ambapo hadi sasa watu wapatao 4000 wamekamatwa hadi kufikia mwisho wa wiki, huku maduka yakiwa yamevamiwa na kuibiwa hasa kutoka maeneo ya Santa Monica hadi Manhattan. 

Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani si jambo jipya na historia inaonyesha hivyo hadi sasa maandamano hayo yamesambaa nchi nzima ndani ya wiki moja kupinga mauaji ya kinyama ya Floyd ambapo licha muuaji wake chauvin kushtakiwa kuuwa bila kukusudia bado waandamanaji wameendelea bila kujali na swali kubwa ni kwanini maandamano bado yanaendelea miji yote nchi nzima?
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...