Huduma kuanza saa 1:00 asubuhi badala ya saa 2:00 asubuhi

Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe imefanya mabadiliko katika utoaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa nje, ambapo muda wa kuanza kutoa matibabu ni saa moja asubuhi badala ya saa mbili asubuhi.

Lengo la uongozi wa hospitali kufanya mabadiliko hayo ni kuboresha huduma za afya ili kuwezesha watu mbalimbali kupata huduma za matibabu mapema zaidi na kwa wakati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Dkt. Paul Lawala amesema mabadiliko hayo yanahusu huduma zote za afya; ikiwamo huduma za afya ya akili pamoja na magonjwa ya mwili.

Dkt. Lawala amesema tangu kuanza kwa utekelezaji wa mabadiliko hayo kumekuwapo na matokeo chanya kwa kuwa watumishi wamefurahia kuanza kutoa huduma mapema, huku wagonjwa na ndugu wakifurahia utaratibu mpya wa kupatiwa huduma mapema na kurejea nyumbani mapema.

“Matokeo chanya yameanza kuonekana kwani watumishi wameitikia wito wa kuwahi mapema na kuanza kutoa huduma saa moja asubuhi.

Hatua hii imesaidia watu mbalimbali kupata huduma za matibabu mapema na kwa wakati na pia watu wengi wamevutiwa na mabadiliko haya,” amesema Dkt. Lawala.

Naye Mkuu wa Kitengo Cha Wagonjwa wa Nje, Dkt. Isack Mrimi amewataka wananchi kufika katika hospitali hiyo kupata huduma za matibabu kwa kuwa Mirembe ina wataalamu wabobezi wenye uwezo wa kutoa huduma bora na kwa wakati.

Huduma za afya katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe zinatolewa na wataalamu wetu ambao wako tayari kukuhudumia wakati wote.
Dkt. Isack Gesase wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe akimsikiliza mmoja wa wagonjwa aliyefika kupatiwa huduma za matibabu katika hospitali hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Dkt. Paul Lawala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...