Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Tigo Tanzania, David Umoh akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kwa njia ya Mtandao wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Tigo Rusha Mapema leo Jijini Dar ES Salaam.
 Kampuni ya mawasiliano inayoongoza kwa kutoa huduma za kidigitali nchini, Tigo Tanzania leo imezindua huduma mpya iliyoboreshwa inayomuwezesha mteja wa Tigo kununua muda wa maongezi pamoja na vifurushi kutoka katika maduka ya Tigo (Tigo shops) na katika maduka ya rejareja yanayotambuliwa na Tigo Tanzania. 

Huduma hii ya Tigo Rusha iliyoboreshwa itatolewa katika mtandao wa mauzo wa Tigo ikiwa ni pamoja na maduka ya Tigo, mawakala wa Tigo Pesa, wauzaji wa kujitegemea, pamoja na katika vituo vya mauzo nchi nzima. Pamoja na huduma nyingine zilizopo, huduma hii itaongeza wigo wa namna ya kuongeza salio kwa wateja.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Tigo Tanzania, David Umoh, amesema, “Kama kampuni inayoongoza kwa huduma za kidigitali, tumejizatiti kuimarisha na kubuni njia zenye kuleta unafuu na zenye chaguzi nyingi ili kumpatia mteja fursa ya kuchagua huduma inayoendana na mahitaji yake kulingana na sehemu aliyopo na muda husika. Tunafanya maboresho haya ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia na maisha kwa ujumla”.

“Wateja wetu wakae mkao wa kula kwamba sasa wataweza kununua muda wa maongezi pamoja na vifurushi kutoka kwenye maduka yetu pamoja na wauzaji wengine wanaotambuliwa na Tigo nchi nzima. Tigo Rusha haina changamoto za kuharibika kwa karatasi ya vocha za kukwangua, lakini pia huduma hii inampunguzia adha mteja wetu wa kutembea na kadi za vocha pindi anapohitaji kuongeza salio kwenye simu yake”.

Tigo Rusha inawapa wateja wetu thamani ya pesa zao kwa maana huduma hii ni rahisi sana kutumia, salama na ya uhakika. Kila mteja wa Tigo atakeyenunua salio au kifurushi chochote kupitia huduma hii ya Tigo Rusha anapewa zawadi ya nyongeza,” ameeleza Umoh.

Umoh pia amegusia manufaa watakayopata wauzaji pamoja na mawakala pindi watakapofanya mauzo yao kwa kutumia njia hii mpya ya Tigo Rusha iliyoboreshwa, pia ameeleza matokeo ya matumizi ya huduma hii kwa maelfu ya wasambazaji wa vocha za kukwangua kote nchini.
“Napenda kuwahakikishia wasambazaji wetu wote wa vocha za kukwangua kwamba hii ni fursa mpya ya kuongeza kipato, hivyo ni fursa pia kwao kukua pamoja na Tigo na kama kampuni tutaendelea kuwaunga mkono wasambazaji wote wa vocha hizo za kukwangua kote Tanzania,” amesema Umoh.

Wateja wote wa Tigo wanashauiriwa kununua muda wa maongezi pamoja na vifurushi kutoka kwa wauzaji na mawakala wa Tigo Rusha ambao wanapatikana katika maeneo yote nchini Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...