Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
RAMON Olorunwa Abass raia wa Nigeria anayeshutumiwa kwa makosa ya udanganyifu amekamatwa akiwa na genge lake wakiwa wamepumzika katika makazi yao huko Dubai, kupitia ukurasa wa Twitter wa polisi Dubai, wamechapisha taarifa na video iliyokuwa inaonesha tukio la ukamtwaji wao.
Abbas ambaye anafahamika zaidi kwa jina la Hushpuppi amekamatwa mapema mwezi Juni akiwa na Olalekan Jacob Ponle marufu kama Woodberry na wengine 10.
Washukiwa 12 wamekamatwa kwa makosa ya kufanya uharifu kwa watu wapatao milioni moja na laki tisa na kusababisha hasara ya zaidi ya Naira 169 bilioni.
Na hiyo ni pamoja na vitu vya thamani yakiwemo magari ya kifahari, simu za mkononi, kompyuta mpakato pamoja na kufanya uharifu katika barua pepe za watu wapatao 800,000.
Kwa miezi minne Polisi wamekuwa wakifuatilia nyendo za wahalifu hao kwa kufuatilia shughuli zao kupitia mitandao yao ya kijamii.
Kupitia video iliyotolewa na polisi, imeelezwa kuwa polisi waliweza kupata eneo walilokuwepo wahalifu hao kupitia shughuli zao katika mitandao ya kijamii.
Polisi wamesema kuwa Hushpuppi na genge lake ni wadukuzi wabobevu katika barua pepe na wamesababisha hasara kwa watu wengi baada ya kudukua miamala na taarifa za kibenki kwa makampuni mbalimbali.
Imeelezwa kuwa waathirika wengi ni raia wa Marekani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...