Chama cha mapinduzi wilayani Ludewa Mkoani Njombe kimesema hakitaki kutumia nguvu nyingi kuwanadi wagombea  wa nafasi ya Ubunge na udiwani, hivyo wagombea hao wanapaswa kuhakikisha wanakubalika katika jamii.

Hayo aliyasema katibu wa chama hicho wilaya Bakari Mfaume katika mkutano wa kamati kuu ya chama hicho uliolenga kujadili utaratibu na mchakato mzima wa uchukuaji fomu za kugombea nafasi hizo.

Alisema kuwa kwa sasa hawataki kukata viuno majukwaani na kuongea sana ili kumfanya akubalike bali watende mambo yatakayowafurahisha wananchi na kuwafanya wawakubali.

Wakati huo huo Mfaume amewataka watia nia kuwa watulivu na kuacha kutoa rushwa ili kupata nafasi ya uongozi kwani kwa kufanya hivyo ni uvunjifu wa sheria na watachukuliwa hatua Kali kisheria.

Aliongeza kuwa wagombea wanapaswa kujitoa katika maendeleo ya wananchi na kutatua kero zao  na si kujininufaisha yeye mwenyewe.

Aidha katibu Huyo aliongeza kuwa katika nafasi ya uraisi Mh. John Pombe Magufuli anatosha na anafaa kuendelea na nafasi hiyo.

Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM)wilayani LudewaMkoani Njombe Bakari Mfaume akiongea na wajumbe wa kamati kuu wilaya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...