Na Karama Kenyunko, Michuzi TV .
JUMLA ya mashahidi 28 akiwemo Mtaalamu kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Hadija Mwema wanatarajia kutoa ushahidi katika kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara Hamis Said Luongo (38) anayedaiwa kumuua mke wake kwa kumchoma na magunia mawili ya mkaa.
Mbali na mashahidi hao, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) atawasilisha mahakamani hapo vielelezo sita ikiwemo ramani ya tukio la mauaji, maelezo ya onyo ya mshitakiwa, ungamo la mshitakiwa kwa mlinzi wa amani, hati ya kuhodhi mali, ripoti ya Mkemi Mkuu wa Serikali.
Hayo yameelezwa leo Juni 26, 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate ambaye amesema kesi ya mshtakiwa huyo itasikilizwa Mahakama Kuu na kwamba ushahidi dhidi yake utatolewa naye atapata nafasi ya kujitetea na kuita mashahidi kama atakuwa nao.
"DPP ameifahamisha Mahakama hii kuwa atatumia vielelezo mbalimbali katika kuendesha ushahidi ambao ni kutoka kwa mashahidi 28 na vielelezo sita," amesema Hakimu Kabate.
Hata hivyo, mshitakiwa alipohojiwa kama atakuwa na utetezi pamoja na mashahidi wa kupeleka mahakamani, Luwonga alidai atajitetea mwenyewe na kwamba hatakuwa na shahidi kwani angeweza kuwaleta ndugu zake na wa upande wa marehemu mke wake kuelezea matatizo yaliyotokea lakini atasimama mwenyewe.
Pia alidai kuwa, ana makovu yaliyosababishwa na kuchomwa visu na mke wake kutokana na ugomvi wa mara kwa mara kati yao lakini hawezi kuyatoa kama kielelezo.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Kabate alisema "Jalada linafungwa na kupelekwa Mahakama Kuu hivyo, utakuwa mahabusu kusubiri kikao kitakachopangwa na Msajili wa Mahakama na utapewa nakala ya jalada la mwenendo wa kesi hii kuanzia ulivyopandishwa kizimbani Julai 30,2019."
Baada ya kueleza hayo, mshtakiwa aliomba tena muongee ambapo alipata ruhusa alidai mahakamani hapo kuwa alimwandikia barua Mfawidhi wa Mahakama hiyo kuhusu ndugu wa upande wa mke wake wamekuwa wakimkataza mtoto wake kwenda Kwa ndugu zake ili waweze kumsomesha kwa kuwa Mali na fedha zipo zitakazosaidia kulipa ada yake ya shule.
"Mtoto wangu anaishi na ndugu wa mke wangu ninaomba mtoto wangu nimuhudumie lakini kinachojitokeza hawa ndugu wanampa maneno ya sumu ili mtoto anichukie,"alidai Luongo.
Katika kesi hiyo ya mauaji namba 4 ya mwaka 2019, mshitakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, mwaka huu akiwa maeneo ya Gezaulole Kigamboni kwa makusudi alimuua mke wake Naomi Marijani kwa kumchoma moto kwa maguia mawili ya Mkaa.
Inakumbukwa kuwa Hamis anadaiwa kumuua mke wake Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.
Mfanyabiashara
Hamis Said Luongo (38) anayedaiwa kumuua mke wake kwa kumchoma na
magunia mawili ya mkaa akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mastaka yanayomkabiri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...