Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo akikabidhi ufunguo wa pikipiki mmoja wa wanakikundi cha Umoja wa Boda baada wa Stendi kupokea mkopo huo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua jana.Picha na Tiganya Vincent.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo akikata utepe kwa ajili ya kukabidhi mkopo wa pikipiki kwa kikundi cha Umoja wa Boda baada wa Stendi iliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua jana
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo akiendesha mmoja ya pikipiki iliyotolewa kwa wanakikundi cha Umoja wa Boda baada wa Stendi na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo akipima joto jana kabla ya kuingia katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akipima joto jana kabla ya kuingia katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo akisaini kitabu cha wageni jana wilayani Kaliua wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo akizungumza jana na viongozi mbalimbali mkoani Tabora kwa kuanza ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ya kukagua shughuli za maendeleo


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dk John Pima akiwasilisha taarifa ya Halmashauri hiyo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo ya kukagua shughuli za maendeleo jana.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu za Mkoa wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo ya kukagua shughuli za maendeleo jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo akizungumza na watumishi wa umma wakati wa ziara yake jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo




NA TIGANYA VINCENT

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua imetoa mikopo ya shilingi milioni 332 kwa vikundi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato yake ya ndani.

Mikopo hiyo imekabidhiwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo kwa niaba ya uongozi wa Halmashauri hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi mikopo hiyo , Mkurugenzi Mtendaji Dkt. John Pima alisema kati ya fedha shilingi milioni 215 kwa vikundi 38.

Alisema wametoa pikipiki 10 zenye thamani ya milioni 25 kwa Kikundi cha Umoja wa Bodaboda Stendi na kukabidhi vifaa vya viwanda kwa vikundi 7 vyenye thamani ya milioni 92.

Dkt. Pima alisema tangu wa fedha ulipoanza hadi hivi sasa wametoa mikipo ya jumla ya shilingi milioni 584 kwa vikundi 99 ambapo vikundi 44 vya wanawake wamepokea milioni 251, vijana vikundi 36 vimepokea milioni 281 na walemavu vikundi 16 vimepokea milioni 51.5.

Kwa upande wa Waziri Jaffo amezitaka Halmashauri nyingine mfano wa Kaliua katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa ajili ya vijana , walemavu na Wanawake.

Alisema Kaliua imeweza kutoa mikopo ambayo itayasaidia makundi hayo kujipatia kipato na kujiletea maendeleo yao na Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...