Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.
Serikali kupitia Wizara ya Maji Nchini ipo mbioni kupeleka huduma ya Majisafi katika Vijiji vinne Katani Kanyigo Wilayani Missenyi, Mkoani Kagera ifikapo Julai Mwaka huu.
Hayo yamebainika katika Ziara iliyofanywa na Mkuu wa Wilaya Missenyi wakati akitembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa maji safi Kata Kanyigo unaohusisha Vijiji vya Kikukwe, Bugombe, Kigarama na Bweyunge, unaotarajiwa kuhudumia Kaya 2,986 sawa na wakazi 10,986 wenye zaidi ya Shilingi Milioni 600.
Akiwa Katika Kijiji cha Kikukwe Mkuu wa Wilaya amejionea utekelezaji wa mradi huo ambao umefikia Asilimia 75, ambapo ametembelea maeneo mbalimbali ya mradi likiwemo nyumba ya mitambo, tanki la kupokea maji ya kisima (sump), ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji n.k
Katika hatua nyingine akizungumza na Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Kigarama Kata Kanyigo, Kanali Mwilla amewaomba Wananchi hao ambao ndio wanufaika wa mradi kuwa tayari kulinda miundo mbinu na kuitunza ikiwa ni sambamba na kukubali kuchangia gharama kidogo za uendeshaji wa mradi huo ambazo ni kulipia umeme n.k, na kwamba wawe tayari kujitolea pale inapobidi ili kuufanya kukamilika kwa wakati.
Pichani ni Jengo la mitambo (pump station) pamoja na tanki la kupokea maji ya kisima lililojengwa eneo la Zahanati Kikukwe Kata Kanyigo Tayari kwa kuwapelekea Maji Wananchi wa Vijiji Vinne vya Kata hiyo Kufikia Julai 2020.
Pichani ni Muonekano wa Tanki la kuhifadhi Maji lenye mita za ujazo wa 130 likiwa tayari limekamilika tayari kwa kupokea maji na kuyasambaza kwa Wananchi.
Pichani Mkuu wa Wilaya Missenyi Kanali Denice Mwilla akipokea Maelezo mafupi kutoka kwa Mhandisi na msimamizi wa Mradi Ndg. Yazidi Bwikizo Mara baada ya kuwasili katika jengo la mitambo ya maji Kata Kanyigo.
Pichani Mkuu wa Wilaya Missenyi Kanali Mwilla akiwa katika moja ya DP inayojengwa katika mradi wa Majisafi Kata Kanyigo, katika Kijiji cha Kigarama ikiwa ni katika kujiridhisha na kazi inayoendelea ya utekelezaji wa mradi huo.
Pichani Mkuu wa Wilaya Missenyi Kanali Denice Mwilla akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wakazi wa Kata Kanyigo Mara baada ya kujionea utekelezaji wa mradi wa Majisafi katika Vijiji vinne Katani humo.
Baadhi ya sehemu ya Wananchi waliohudhuria katika Kikao maalumu wakiendelea kumsikiliza Mkuu wa Wilaya Missenyi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...