Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof.
Kitila Mkumbo akizindua eneo la kunawa mikono katika kukabiliana na
maambukizi ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona (COVID-19)
katika shule ya sekondari ya Tumaini, mkoani Singida ambapo wanafunzi
zaidi ya 100 wanajiandaa kwa mtihani wa kidato cha Sita. Kulia kwake
anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula.

Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof.
Kitila Mkumbo akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Tumaini
wanaojiandaa na mtihani wa kidato cha Sita ambao amewakabidhi
vitakasamikono ambavyo kila mmoja ataweza kutumia kwa muda wa siku 60.
Aidha, jumuiya ya shule hiyo pia ameikabidhi miundombinu ya kunawa
mikono

Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof.
Kitila Mkumbo (kushoto) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa shule ya
sekondari ya Tumaini vitakasamikono kwa niaba ya jumuiya ya shule hiyo
katika hafla fupi ya kukabidhi miundombinu ya kunawa mikono na
vitakasamikono iliyofanyika shuleni hapo.

Sehemu ya vitakasamikono ambavyo
wanafunzi wa shule ya sekondari ya Tumaini, mkoani Singida wamekabidhiwa
. Vitakasamikono hivyo vimeandaliwa Idara ya Ubora wa Maji, Wizara ya
Maji, ni moja ya mchango wa sekta ya maji katika mapambano dhidi ya
kujikinga na maambukizi ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...