IKIWA dunia bado inaendelea na mapambano dhidi ya mlipuko wa janga la virusi vya Corona (Covid-19) wito pia umetolewa na Umoja wa mataifa katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yanayoadhimishwa Juni tano kila mwaka huku kwa mwaka 2020 yakiwa yamebeba kauli mbiu ya "Bayoanuai."
Katika maadhimisho hayo shirika la ndege la Emirates, likijua vizuri jukumu lake katika mfumo wa ikolojia kidunia limeendelea kufanya maendeleo katika kufikia malengo yake ya mazingira, ambapo limeonesha utendaji katika sekta ya mazingira hayo katika ripoti yake ya fedha kwa mwaka wa 2019/2020 ambapo picha kamili na muktadha wa mafanikio yake yameelezwa vyema.
Shirika la Emirates limeeleza kuweka umuhimu kwa kuwaweka salama wanyama wa porini ambapo Shirika hilo limeeleza limedhamiria na kuendelea kujitolea kushughulikia biashara haramu hasa uuzaji wa wanyamapori au viungo vyao aidha kwa chakula, dawa, mapambo, vito, pembe au ngozi huku vyote vikigharimu sekta hiyo dola za kimarekani bilioni 20 kila mwaka.
Emirates imekua ikifanya kazi kwa ukaribu na mashirika ya kimataifa na hiyo ni pamoja na kuwa sehemu ya umoja wa kimataifa kwa wanyamapori na wamekuwa na mchango mkubwa katika kusimamia sheria dhidi ya usafirishaji wanyama kwa njia haramu hasa wale waliokuwa hatarini kupotea na pia ni washirika wa Baraza la usafiri na utalii (WTTC.)
Shirika hilo limeeleza kuwa hawana uvumilivu kwa wabeba wanyama waliopigwa marufuku, nyara za uwindaji au bidhaa yoyote inayohusiana na shughuli haramu za wanyamapori huku ikielezwa kuwa timu ya masuala hayo imepata mafunzo ya kanuni za moja kwa moja za wanyama pamoja na sera zake za ndani, na wafanyakazi zaidi ya 2,500 walipata mafunzo hayo mwaka jana yakiwemo kutambua na kuripoti mizigo inayoshukiwa pamoja na kujenga ufahamu kwa wateja kuhusiana na kuacha biashara haramu kupitia programu mbalimbali.
Imeelezwa kuwa juhudi za Emirates katika maeneo ya uhifadhi wa wanyamapori zinajulikana kwa umma na Shirika hilo limekuwa likisaidia kulinda mimea adhimu (Flora na Fauna ) nchini Australia kwa zaidi ya miaka 10 na hiyo ni pamoja na eneo la bonde la Emirates Wolgan, na eneo la New South Wales Resort ambako wamefanya kazi kwa karibu na jamii ya eneo hilo ili kuweza kuwahamishia hapo wanyama waliokuwa hatarini kutokana na uchomaji wa misitu ambapo hadi sasa wanyama wengi wakiwemo Kangaroo wamerejea katika eneo hilo.
Emirates imekuwa na ushirikiano wa miaka 20 na Hifadhi ya Jangwa la Dubai (DDCR) na wamendelea kuendesha programu zilizozaa matunda hasa katika kufuatilia, kutunza na kuanzisha spishi mpya za wanyama wa porini kama vile Arabian oryx na Arabian gazelle ambapo hadi kufikia Januari mwaka huu hifadhi hiyo ilifanikiwa kutoa spishi zaidi ya 250 asili (MacQueen's bustards.) huku wakiendela kufanya utafiti za ikolojia kwa kushirikiana kikamilifu na vyuo vikuu vya ndani na kimataifa hali iliyopelekea kuwa moja ya maeneo ya hifadhi yaliyokidhi viwango na yanayosimamiwa vizuri ulimwenguni kwa mwaka 2018.
Katika suala la kusimamia upunguzaji wa uzalishaji wa kaboni limekuwa suala la msingi katika mkakati wa kudumisha mazingira wa Emirates, ambapo kumekuwa na programu za kimkakati kwa usalama katika sekta hiyo ya anga, ambapo programu ya ufanisi wa mafuta ya ndege ambayo inachambua na kutekeleza njia za kupunguza uchomaji wa mafuta usio wa lazima na uzalishaji ilileta uboreshaji wa asilimia 1.9 katika ufanisi wa mafuta kwa ndege za abiria.
Emirates imedhamiria kuwa mabalozi bora wa mazingira, pamoja na kushirikiana Serikali na wadau katika makubaliano na mabadiliko katika mfumo wake wa mazingira sambamba na kutunga na kusimamia sera za ndani ili kuendelea kuiweka salama sekta hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...