MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Kheri James ametangaza kuwarejesha katika majukumu yao ya uongozi vijana sita waliosimamishwa uongozi Ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma za kupokea na kutoa Rushwa zilizokuwa zinawakabili.

Kheri amesema iamuzi huo umefikiwa baada ya Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi (ZAECA) iliyopewa jukumu la kuchunguza tuhuma dhidi yao kuonyesha kuwa vijana hao hawakuhusika katika tuhuma hizo.

Akizungumza na leo jijini Dodoma, Kheri amesema Mwezi Mei alitoa uamuzi ulioafikiwa katika kikao cha kamati ya utekelezaji ya jumuiya hiyo wa kuwasimamisha viongozi hao Ili kupisha uchunguzi ambapo alisema endapo ikibainika wamehusika wachukuliwe hatua za kisheria na kama hawakuhusika  wataendelea na majukumu yao.

Amewataja vijana hao kuwa ni mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kaskazini Unguja Pandu Salum Sungura, Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Lulu Mwacha na  Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Amina Bakari Yussuph.

Viongozi wengine ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa kaskazini Unguja Alawi Khaidar Foum, Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Mkoa wa Mjini Hussein Ayoub Iddi na Mjumbe wa Baraza kuu Mkoa wa mjini Fransisca Camchus Clement.

Kheri  amekemea siasa za kutwezwana,kukejeli na kuwadhalilisha baadhi ya wanachama waliojitokeza kuomba ridhaa kwa CCM kugombea nafasi ya Urais katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kisa tu walihudumu katika serikali au taasisi nyingine.

Amewataka vijana wenye sifa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali hasa za udiwani ambapo ndio chimbuko la maendeleo ili wawe sehemu ya kusukuma mambo yanayohusu vijana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...