Janga la ugonjwa wa virusi vya COVID-19 umeleta uhaba ya bidhaa nyingi humu nchini zikiwemo Barakoa. Rania Nasser ambaye ni mwanafunzi wa sekondari aliunda kikundi kinachojulikana kama Barakoa Tz cha kutengeneza na kugawa barakoa bure kwa wale wenye uhitaji. Nia yake kubwa ilikuwa ni kutengeneza barakoa nyingi na kuzigawa bure kwenye vituo vya polisi vilivyo karibu na nyumbani kwao bure kabisa.

Baada ya wiki moja, uhitaji wa barakoa uliongezeka maradufu na hivyo akaona umuhimu wake ukiongezeka. Kwa sababu hiyo, ilimlazimu kuomba uzaidizi kwa marafiki na ndugu zake wa karibu ili kukabiliana na uhitaji wa barakoa.

Kwa sasa imekuwa ni wiki kadhaa tangu kuanzishwa kwa kikundi cha Barakoa Tz na tayari washatengeneza na kugawa zaidi ya barakoa 1,000 kwenye vituo vya mayatima, wahudumu wa afya, polisi lakini zaidi kwa wale wenye uhitaji. Hii imefanikiwa kutokana na kutumia muda mrefu kwenye kushona barakoa kutoka kwa wasamaria wema pamoja na wafadhili.

Rania kwa sasa anao wasamaria wema pamoja. Kuna baadhi ya wasamaria ambao wanashona barakoa mkoani Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam pamoja na kusambaza kote mtaani. Lakini pamoja na kuwa na wasamaria wema wengi hivyo, Rania anaomba wengine wajitokeze. Rania anasema ‘Hata kama huwezi kushona kwa haraka, hiyo haina shida ni sawa kwani barakoa moja inaweza kuokoa maisha ya watu wengi.’

 Linapokuja suala la aina  ya kitambaa cha kushona, Rania anasema yeye hupata aina zote tofauti za mifumo na atachukua kitambaa cha aina yoyote ambacho anaweza kupata. Jambo moja la kuhakikisha ni kwamba ni pamba. Kitambaa cha kunyoosha kinaruhusu chembe zaidi kupita katikati, ambayo sio kile unachotaka kwa ajili ya kufunika uso. Kwa sasa yeye anatengeneza barakoa nyingi kwa ajili ya watot na anatoa wito kwa wenye miundo zaidi ya kitambaa cha watoto au mifumo mingine washirikiane ili kuja na aina mbali mbali tofauti.

Jambo lingine Barakoa Tz wanatarajia kutoa ni vifaa vidogo ambapo familia zinaweza kujishonea barakoa zaowenyewe. Rania Nasser alisema ni jambo rahisi sana kuweka pamoja na atatoa vifaa hivyo na maelekezo kwa watu kote Dar es salaam.
Rania Nasser stitching Masks.
 Rania Nasser donating Masks at Mother Theresa Charity Center
 Rania Nasser donating Masks at Msimbazi Orphanage
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...