Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema baada ya Rais Dk.John Magufuli kutangaza kufunguliwa kwa shule zote Juni 29,2020, yeye leo hii hatalala kuhakikisha anapanga ratiba yote ya mitihani ya darasa la nne, darasa la saba na kidato cha nne.
Ametumia pia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa sasa hali ni shwari na uamuzi wa shule kufunguliwa Juni 2020 umemfurahisha hivyo wanafunzi wajiandae na mchakamchaka wa masomo utakaoanza jumatatu.
Akizungumza leo Juni 16, Bungeni Mjini Dodoma Profesa Ndalichako mara baada ya kuvunjwa kwa kikao cha 11 cha Bunge Ndalichako amesema kuwa, amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa walimu, wazazi na hata wamiliki wa shule hasa binafsi waliokuwa wakiuliza lini shule zitafunguliwa na hiyo ni kutokana na ushwari wa hali ya virusi vya Corona.
Aidha amesema wanafunzi waliopo katika madarasa ya mitihani watumie muda uliobakia kulala na baada hapo kazi yao itakuwa ni kusoma tu, iwe iwe mchana ili kwenda na ratiba kwani hataki kuoa muhula unaharibika."Mpaka Desemba mwaka huu tuwe tumalimaliza masomo yote tena kwa wakati.
" Na leo sitalala hadi nihakikishe ratiba za mitihani kwa darasa la nne, la saba na kidato cha nne imekamilika hivyo wanafunzi wajiandae katika mchakamchaka huo ili kufidia muda" amesema.
Kuhusu visa vya Corona tangu kidato cha sita na vyuo kufunguliwa Profesa Ndalichako amesema hakuna kisa chochote cha Corona kilichoripotiwa.
"Wanafunzi walioripoti wanaendelea vyema na masomo yao na hakuna kisa kilichoripotiwa hadi sasa, hivyo hakuna sababu ya wanafunzi kuendelea kubaki nyumbani hivyo wajiandae kurejea mashuleni kuendelea na masomo" amesema Ndalichako.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...