Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
RAIS Dkt. John Magufuli amesema kuwa Uchaguzi Mkuu unaotegemewa kufanyika Oktoba mwaka huu utakuwa huru na haki kwa vyama vyote huku akitahadharisha wale wote watakaoleta vurugu na kauli za matusi watambue Serikali ipo macho na haitovumilia.

Akizungumza leo Juni 16,2020 jijini Dodoma wakati akifunga Bunge la 11, Rais Magufuli amesema kuwa uchaguzi huo utakua wa huru na haki kwa kuwa ndio Demokrasia huku akivitaka vyama kutoa nafasi za kugombea kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu katika nafasi hizo za uwakilishi.

Aidha amesema kuwa chaguzi lazima zifanyike kwa amani bila kuendeleza matusi na kejeli kwa kuwa havijengi na amevishauri vyama vya siasa kubishana kwa hoja na kushindanisha ilani.

Rais Dkt.Magufuli wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ushirikiano na kuiunga mkono Serikali na kudhihirisha kauli ya, "Uchungu  wa Mwana aujuaye mzazi" na amewashukuru wabunge wa vyama pinzani walioonesha ushirikiano licha ya kuwa na itikadi tofauti na kueleza kuwa wale waliokuwa wakipinga kila kitu mhula ujao watakuwa wamejifunza kupingapinga sio kuzuri.

Pia Rais Magufuli amemshukuru Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein ambaye pia amemaliza muhula wake na kueleza kuwa amefanya kazi katika kutumikia umma kwa kiasi kikubwa sana na amehaidi kumuenzi kama viongozi wengine.

Aidha amekishukuru chama cha Mapinduzi kwa Kuhakikisha ilani inasimamiwa vyema katika kulipeleka mbele taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...