Na Woinde Shizza , michuzi Tv Arusha.
Waziri wa Ardhi nyumba na makazi William Lukuvi amewataka maafisa ardhi kuwapa hati Mara moja watu wote waliopimiwa viwanja ili idadi iliyo kwenye michoro iwe na hati kwa ajili ya kuondoa migogoro.
Aidha aliwataka watu wote walio mjini kuanzia kuchukuwa hati za nyumba zao ili kuondokana na ulofa ambapo watambue kuwa hakuna makazi holela hivyo hati hizo kuwasaidia kupata mikopo kwenye taasisi za kifedha.
Aliyasema hayo wakati akizindua ofisi ya Ardhi mkoa wa Arusha zilizopo kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha nakuwataka kuacha madalali wa Ardhi kutumia ofisi za ardhi na kuwatapeli wananchi.
Alisema kuwa hataki makandokando kwenye ofisi za ardhi kwani Kuna baadhi ya maafisa huwatumia makanjanja kutoa taarifa za ardhi wakiwa Chini ya mti na baadaye haohao ndio hutumika kuwakusanyia fedha.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha ametakiwa kufanya tathmini ya Watendaji wake ili kubaini ambao hawatendi haki na wajibu wao ili kuwaondoa Mara moja na kuchagua wengine ambao wataweza kwenda na kasi ya awamu ya tano
Hata hivyo ameweza kumfukuza kazi afisa ardhi aliewahi kufanya kazi katika halmashauri ya Meru Nicodemas Hiru kwa kitendo Cha kumpa ardhi yenye hekari 3000 na kuingizia serikali asara ya shilingi milioni miatano kwa kulipa fidia wakati huo huo alimpandisha cheo aliekuwa afisa ardhi halmashauri ya Arusha ,nakumfanya kuwa afisa ardhi katika jiji la Arusha Rehema Jato
Lukuvi akiongelea swala la kiwanja Cha Standi kilichokuwa na mgogoro mda mrefu na hati yake ulikuwa haionekani kwa Sasa ipo na yeye ndio alikichukuwa hivyo alitumia muda huo kumuagiza kamishina was Ardhi wa mkoa wa Arusha kuchukuwa hati hiyo na kumkabidhi mkurugenzi mpya wa halmashauri ya jiji la Arusha kwa ajili ya ujenzi huo.
"Mkurugenzi wa jiji nakupa hati ujenge Standi katika eneo la Bondeni city eneo Hilo utalipia fidia Wala kulipiana fedha za kujenga Standi hiyo utazipata tu "alibainisha Lukuvi
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Kimanta alisema kuwa ofisi ya Ardhi kumekuwa na changamoto nyingi ikiwepo ya eneo la ofisi kwa ajili ya kuhifadhia taarifa za wananchi hivyo aliwahaidi Ndani ya wiki moja atakuwa amewapatia eneo ambapo alimuagiza katibu Tawala mkoa wa Arusha kupitia viwanja vyake na Hadi ifikapo ijumaa awe ameshampatia eneo
Alisema kuwa kwa sasa yupo tayari kufanya kazi na mwananchi yeyote ambaye anakero aipeleke ofisini kwakwe siku yoyote atazitatua na hata weka siku ya kusikiliza kero hizo Bali mwananchi yeyote mwenye shida aipeleke mkoani,huku aliwataka Watendaji wa serikali kubadilika.
Waziri wa Ardhi nyumba na makazi William Lukuvi akionyesha ramani inayoonyesha mipaka ya Wilaya zilizopo mkoa wa Arusha .
Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Kimanta akiongea katika uzinduzi wa was ofisi ya mkuu wa mkaoa was Arusha.
Waziri Lukuvi akiongoa katika uzinduzi wa ofisi ya Ardhi mkoa wa Arusha
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...