Na mwandishi wetu, Arusha
MADAKTARI waliokuwa wakishiriki mafunzo ya siku tano ya uelimishaji wa tathmini za ulemavu utokanao na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini, wamefurahishwa na elimu waliyoipata na kwamba itasaidia kutenda haki kwa pande zote mbili, wanufaika na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Mafunzo hayo yaliyoanza Juni 22, 2020 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) jijini Arusha yaliandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambapo zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga walijifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sheria iliyoanzisha Mfuko, jinsi Mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na kazi anavyoweza kuwasilisha madai, jinsi ya kufanya tathmini ya ulemavu uliotokana na ajali au ugonjwa utokanao na kazi.

“Katika mafunzo haya nipende kusema kwamba wakufunzi wamekuwa makini sana na wamefundisha kile ambacho kilistahili na kila mmoja amekiri kuwa wakufunzi wamefanya kazi nzuri na hata mazoezi ya vitendo kwa washiriki hakuna aliyepwaya.” Alisema Dkt. Peter  Mabula ambaye ni mwenyekiti wa washiriki.

Alisema mafunzo hayo yamewaandaa kwenda kufanya kazi nzuri kuliko ile ambayo walikuwa wakifanya hapo kabla.


“Mafunzo haya yametuandaa kwenda kutenda haki kwa wagonjwa wetu na kwa Mfuko, wale wagonjwa wanaokuja kwetu hatimaye wanakuja kupata fidia hivyo tumejifunza umakini wa kufanya tathmini kwa umakini na ubora ili kutouibia mfuko au kumuibia wateja na hivyo sisi tunasimama katikati
ya wateja na mfuko ili tuweze kutenda haki.” Alisema Dkt. Mabula.


Akitoa hotuba ya kufunga mafunzo hayo Dkt. Omar Chande kwa niaba ya mganga mkuu wa Mkoa wa Arusha alipongeza hatua ya Mfuko kuongeza idadi ya wataalamu watakaoweza kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji kulipwa fidia.

“Fursa hii ya utoaji mafunzo imekuja wakati muafaka na ni imani yangu kile
kilichofundishwa hapa ndicho kitakachokwenda kuondoa changamoto za watu ambao hapo awali walipata shida inapofikia wakati wa kudai fidia.” Alisema Dkt. Chande.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary alisema mwaka 2015 Mfuko kupitia usaidizi wa Shirika la Kazi Duniani uliweza kutoa mafunzo kama haya kwa madaktari 346 na hadi kufikia Ijumaa Juni 26, 2020 madaktari wanaokaribia 1,000 tayari wamepatiwa mafunzo.
Daktari akionyesha stika atakayobandika kwenye hospitali anakotoka kuonyesha huduma za WCF zinapatikana kwenye hospitali husika, wakati wa kufungwa kwa mafunzo hayo.
Baadhi ya madaktari wakionyesha stika watakayobandikwa kwenye hospitali wanakotoka kuonyesha huduma za WCF zinapatikana kwenye hospitali hizo, wakati w akufungwa kwa mafunzo hayo
Dkt. Nancy Shuma (kushoto) kwa niaba ya washiriki wenzake akikabidhiwa stika itakayobandikwa kwenye hospitali anayofanyia kazi kuonyesha huduma za WCF zinapatikana kwenye hospitali husika. Anayemkabidhi ni Mkuu w akitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa umma WCF, Laura Kunenge.
Dkt. Omar Chande (wapili kushoto), kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha akikabidhio vyeti kwa washiriki.
Dkt. Peter Mabula akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Dkt. Omar Chande, akitoa hotuba ya kufunga mafunzo kwaniaba ya mganga mkuu wa mkoa wa Arusha.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Om
Dkt. Pascal M agesa, Afisa madai na tathmini WCF.
Dkt. Ali Mtulia, Meneja anayeshughulikia madai na Tathmini WCF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...