Na Mwandishi wetu Shinyanga
MAKAMU wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali Idd amewaonya baadhi ya
wanachama wa chama cha Mapinduzi wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi kupitia chama hicho kujiepusha na matumizi ya fedha katika
kutafuta nafasi za uongozi kwani kufanya hivyo ni kukiuka katiba ya
Chama hicho.
Aidha
Barozi Seif Ali Idd ameonya kuwa kuna baadhi ya watu wenye nia ya
kugombea uongozi lakini badala ya kwenda wenyewe wanatuma watu wengine
kutoa rushwa kwa niaba yao nakuonya kuwa wana taarifa zao na
watashughulikia ipasavyo kwani watu wanonunua uongozi sio watu wazuri
hata kidogo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali Idd ameyasema hayo leo
wakati wa ziara yake ya kichama Mkoani Shinyanga alipokutana na viongozi
wa Chama Cha Mapinduzi wa Mkoa na Wilaya ya Kahama kama mlezi wa Chama
cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga.
‘’Kiongozi
yoyote anayetafuta uongozi kwa kwa kununua huyo sio kiongozi mzuri,
uongozi hautafutwi kwa kununua bali uongozi utafutwa kwa kujenga hoja’’.
Aliendelea kusema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali
Idd.
Aidha
Kiongozi huyo mkubwa Nchini amesisitiza kuwa serikali iko macho sana
kuwabaini wale wote wanaotaka kutumia ushawishi wa fedha kujipatia
uongozi kwani macho yake yanaangaza kila mahali na wana uhakika kuwa
wataonekana pasiposhaka na kuwataka kuacha siasa za namna hiyo mara
moja.
Barozi
Seif Ali Idd amesema mtu akiwaletea viburungutu vya fedha kwa lengo la
kununua uongozi chukueni lakini msiwachague maana unaweza kukosea
kuchagua na ukajikuta unachagua uhalifu katika jimbo kwani kiongozi
anayechaguliwa kwa rushwa ni mhalifu kama walivyo waalifu wengine.
Aidha
Barozi Idd amewataka wabunge Mkoani Shinyanga kuendelea na kazi ya
kukamilisha ahadi zao kwa wananchi kwani bado ni viongozi mpaka zoezi
lakuchukua fomu litakapoanza ingawa inawezakena baadhi yao wanaweza kuwa
wanamaliza muda wao na wengine kupoteza nafasi za uongozi kwa kushindwa
katika kura za maoni.
‘’Achaneni
nao viongozi wanaotumia fedha kutimiza ahadi ya chama cha mapinduzi
ambayo inataka mgombea kupita bila matumizi ya rushwa na tamaa.
Ukumpitisha kiongozi wa rushwa maana yake umepitisha uovu kwenye
jimbo’’. Alionya Makamu wa Rais wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Idd.
Aidha
kiongozi huyo ameonya kuwa kwasasa kuna baadhi ya wanachama wa Chama
Cha Mapinduzi na baadhi ya watu serikalini wanaojifanya madalali wa
wagombea na wanawahamasisha baadhi ya watu kwenda kugombea nafasi ya
uongozi na kuonya kuwa tabia hii pia haikubaliki kwani uongozi ni suala
la hiari.
Katika
salam zake kwa wanachama wa chama cha Mapinduzi Mkoani Shinyanga Mbunge
wa Kahama Jumanne Kishimba amemwomba Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Barozi Seif Ali Idd kuangalia namna bora ya kuwapa motisha hata
kuwapatia Bima za Afya kutokana na juhudi zao katika kujenga Chama Cha
Mapinduzi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar yuko Mkoani Shinyanga kwa ziara ya Kichama
na ataendelea ziara yake katika Manispaa ya Shinyanga na kuendelea
kufanya shughuli za Chama kwa kuwa ni mlezi wa Chama hicho Mkoani
Shinyanga.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali Idd akiongea wakati wa
ziara yake ya kichama Mkoani Shinyanga alipokutana na viongozi wa Chama
Cha Mapinduzi wa Mkoa na Wilaya ya Kahama kama mlezi wa Chama cha
Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akifuatilia kwa makini hotuba ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Barozi Seif Ali Idd wakati wa ziara
yake ya kichama Mkoani Shinyanga alipokutana na viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi wa Mkoani humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...