MBUNGE wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwan Kikwete, amekabidhi vifaa tiba katika kituo cha afya
cha Miono,Mkoani Pwani vilivyotolewa kwa hisani ya taasisi ya kifedha ya
Stanbic.
Akikabidhi
vifaa hivyo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya chalinze,alisema vifaa hivi
vitakuwa neema na mkombozi kwa mahitaji wa afya kutokana na baada ya
ukamilikaji wa chumba cha Upasuaji ambacho kitahudumia wananchi wa
maeneo hayo hususan wakina mama wakati wa kujifungua na huduma za
upasuaji.
"Nimekuwa
nikikosa usingizi nilipoona kituo hiki cha Miono kinasuasa kwisha.
Lakini nashukuru Serikali kupitia Halmashauri yetu imetoa pesa na sasa
kituo kipo hatua ya mwisho ya ujenzi."
Ridhiwani
hakusita kumshukuru Rais John Magufuli na serikali ya awamu ya Tano kwa
namna inavyoendelea kuimarisha afya za wananchi kwa kuwapatia zaidi ya
sh. Bilioni 1.7 ambazo Zimetumika kwa ajili ya miradi mbalimbali ya
Kuimarisha afya katika kata mbalimbali za halmashauri hiyo
"Ujenzi
wa kituo cha afya cha kiasasa Kata ya kibindu, kituo cha Afya cha
Lugoba, Miradi ya upanuzi wa kituo cha Afya Chalinze sanjari na ujenzi
wa Maabara kubwa ya damu, kituo cha ushauri nasaha Mdaula na Zahanati ya
Kijiji cha Mdaula" alibainisha Ridhiwani.
Nae
Meneja wa Stanibic Bank ,Richard Chenga alimpongeza mbunge huyo kwa
jinsi anavyokuwa mstari wa mbele kuwasemea watu wake na jinsi
anavyovumbua miradi yenye tija kwa wananchi wake.
Alizitaka
taasisi nyengine nchini kuunga mkono juhudi za serikali katika
kusaidia jamii ususani ni uyaratibu wa kutoa magawio kwa wananchi ili
kuunga mkono serikali katika utekelezaji wake wa miradi.
Halima
Juma,ni mkazi wa Miono alimpongeza Mbunge Ridhiwani kwani kwa kufanya
hivyo wakina mama wa watakuwa wanajifungua bila matatizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...