Mkuu wa kitengo cha Ustawi wa
Jamii na Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Salum
akimkabidhi Mr. Jackson Msilambo Tsh. 4,370,000/= zilizotolewa na
Mchungaji Rose Shaboka kutoka kanisa la New Day Church kwa ajili ya
gharama za matibabu ya mtoto wake anayetibiwa JKCI leo Jijini Dar es
Salaam.

Baba wa mtoto anayetibiwa katika
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mr. Jackson Msilambo akimpa mkono
wa shukrani Mchungaji Rose Shaboka kutoka kanisa la New Day Church baada
ya kukabidhiwa Tsh. 4,370,000 kwa ajili ya gharama za matibabu ya mtoto
wake anayetibiwa JKCI leo Jijini Dar es Salaam

Mchungaji wa kanisa la New Day
Church Rose Shaboka akimjulia hali mtoto wa Jackson Msilambo baada ya
kuchangia gharama za matibabu ya mtoto huyo anayetibiwa katika Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo Jijini Dar es Salaam. Pia Mchungaji
Rose amechangia kiasi cha Tsh. 500,000/= kama gharama za matibabu pamoja
na gharama za kupatiwa bima ya afya kwa mtoto mwingine anayetibiwa
JKCI.
Picha na: JKCI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...