Na Khadija Seif, Michuzi tv

ZAO la mashindano ya BSS Menina Atick amewaomba wasanii kusaidia jamii hasa wamama pamoja na watoto.

Menina amesema hatosita kuwasaidia wamama pamoja na watoto wanaopitia changamoto za kiafya.

"Ifike wakati wasanii na watu mashughuli waiona fursa ya kusaidia jamii hasa wamama ambao wanapitia changamoto ya kujifungua pamoja na watoto wanaozaliwa na matatizo hasa watoto njiti,"

Hata hivyo Menina amesema mbali na kutembelea hospitali hiyo ya vijibweni katika wilaya ya kigamboni jijini Dar es salaam na kuwapatia wamama vipimio joto,gloves,kiti cha kubebea wagonjwa, mabeseni pamoja pempasi, ameamua kukarabati chumba cha watoto njiti.

"Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati Yani njiti wanahaki ya kuishi hivyo nimechukua jukumu la kutengeneza chumba cha watoto hao ili waweze kukua vizuri,"Pia,amesema zoezi la kusaidia wamama pamoja watoto litakua endelevu kwa Kila hospitali.
Menina Atick akikabidhi vifaa kwa madaktari wa wodi ya wazazi katika hospitali ya serikali ya vijibweni 
Msanii wa Bongofleva Menina Atick akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea hospitali ya vijibweni katika wilaya ya kigamboni ikiwa ni sehemu ya kampeni yake ya kusaidia akina Mama pamoja na watoto njiti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...