
Mkutano Maalum wa 41 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki utafanyika tarehe 4 na 5 Juni 2020 kwa njia ya mtandao (Video Conference). Mkutano utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara uliopo Mji wa Serikali, Mtumba – Dodoma.
Mkutano huo Maalum wa 41 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki, utaanza kwa mkutano wa ngazi ya wataalam tarehe 4 Juni, 2020 na kufuatiwa na mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu tarehe 5 Juni 2020 na kisha kufuatiwa na mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki siku hiyohiyo (kuanzia
saa 9:00 alasiri hadi saa 11:00 jioni).
Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo utajadili masuala ya fedha na utawala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...