Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (katikati), kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nchi George Simbachawene na mwisho kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi, Dkt. Faraji Mnyepe wakifuatilia mkutano kwa njia ya video conference, Jijini Dar es salaam.

Mawaziri pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu/Maafisa waandamizi kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano kwa njia ya Video Conference, jijini Dar es Salaam

Mkutano ukiendelea

*********************************

Mkutano wa Mawaziri wa Kamati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama kwa ngazi ya Mawaziri umefanyika kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing) na kujadili masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama.

Mkutano huo umefanyika chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhe. Sibusiso Busi Moyo na utakutanisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mambo ya Ndani, Ulinzi pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka nchi wanachama wa SADC. Ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi.

Mkutano huo umehudhuriwa na nchi 16 wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Afrika Kusini, Botswana, Comoro, DRC, Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...